Sehemu Ya 1
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Inapoanzia Rasmiiii
STORY HII INAITWA SECONDARY SCHOOL AU KWA KISWAHILI NI
( SHULE YA UPILI ).....
KWAHIO PIA WAWEZA KUIITA HIVYO TU BASI
Story hiii mimi ni mtoto wa kitajiri ile mbaya... na wakiume nipo mimi mwenyewe na nina dada zangu wawili wenye asili ya kiarabu. kwani mama yangu yeye pia ana asili ya kiarabu.....
Ninae dada yangu ambae ana umri wa miaka 25 huyo ni wa kwanza na keshamaliza shule muda tu... kisha ninae dada yangu mwingine ambae tumefuatana.. yeye ana umri wa miaka 22 na yeye bado yupo kidato cha 4... afu anafatiwa na mimi kidume sharbiny rashidy mwenye umri wa miaka 20 na yupo kidato cha 3.... familia yetu ilikua ni familia ya kitajiri sana yaani tulikua ni matajiri waliopindukia....
Ila katika watoto wote wa mzee rashidy mimi peke yangu ndio nilikua nina rangi tofauti na dada zangu wote. Ila nyumba yetu imezungukwa na wafanyakazi wengi mno. kama kwa raisi vile kumbe ni kwa mtu tu wa kawaida...
"mwanangu utaenda kesho tu"
"mamaa mi sijawahi kukosa kwenda shule hivyo nisipoenda naisi kama nitaumwa yani"
"mmhh haya ila njoo unywe chai basi"
"nitakula huko huko mamaa"
"mwajabu? we mwajabu?"
"abee dada?"
"umeona mtoto wangu anaenda shule na njaa?"
ndani kwetu tulikua tuna mfanyakazi ambae ni mtu mzima kabisa na ndio alionilea mimi toka nikiwa mtoto.... hivyo roho inaniuma sana pindi ninapoona anafokewa kwa ajili yangu,
"kakaa njoo unywe chai"
Aliniita yule mdada wa makamo kabisa tena hata sio mdada ni mmama kabisa. kwani alitulea mimi na dada zangu wote, lakini dada zangu asa huyu mdogo hua hamueshimu huyu mama na sijui ni kwanini....
"mamii nimeshiba usijali"
Nilimuambia kwa kwa utaratibu na heshma zote alizonilea yeye mwenyewe.
"sheby mwanangu?"
"sema ukirudi unataka ule chakula gani?"
Alioniuliza ni mama yangu mzazi
"aaaa chochote tu mamaa"
"yaani we mwajabu humuulizi mtoto atakula nini umeuchubua tu"
"mamaa mbona ivyo lakini?"
"amna mwanangu ni huyu mtu naona hakujali kabisa yani"
"ok nitakula ugali na mrenda"
"haaaaaaa sheby mwanga chakula gani hicho cha kishenzi hivyo?"
"mamaa kwani hicho mbona pia ni chakula"
Mara mami kazi akaingilia kati
"lakini dada kama kapenda mwenyewe kula labda tumuache tu"
"hapana mwanangu hawezi kula matapu tapu hayo... afu wewe mwajabu umenilelea mtoto wangu vibaya sana wewe"
"nisamee dada"
Nilichukua BMX yagu ambayo hua naendaga nayo shule pindi ninapopitwa na school bus, Hua shule ninayosoma ni shule ya serikali iitwayo
ASHRAF SEMINARY SEC SCHOOL ni shule ya kiislamu ambayo ina maadili mema kila idara....
Shuleni mimi ni mtu ambae sina kosa hata moja kutokana na heshma na upole nilionao... mimi nasoma katika shule hio ya kiislamu ambayo ambayo ina maadili mema kede kede....
Na dada yangu ZAITUNI yeye anasoma katika shule nyingine tofauti na hiii.... hio anayosoma dada yangu zaituni ni shule ya private na ya kitajiri tuuu yaani kama una utajiri wa mawazo huezi kusoma katika shule hio iitwayo ST PETER SUNEKA SECONDARY
**********************************
HIII SHULE NILISOMEA KENYA KIUKWELI UKWELI ILA KWENYE HII STORY NITAIFANYA KAMA IPO ARUSHA VILE...... SASA MSIJE MKANIKOSOA NA KUNIAMBIA oohh mbona hio shule ipo kenya...SASA MJUE KUA HIO SHULE NILIISOMEA KWELI KWELI NAIROBI KENYA ILA KWA HII STORI NITAIFANYA KAMA IPO ARUSHA VILE.... YAANI KISTORY STORY IWE ARUSHA LAKINI KIUKWELI IPO KENYA SEHEMU IITWAYO ~KISII~ NA NILISOMEA HIO SHULE KIUKWELI ILA SIO YA UTAJIRI KIHIVYO
**********************************
Sasa dada yangu ndio anasomea shule hio ya kitajiri ambayo wanafuzi wao huenda na simu na magari kabisaaa.... tena hio shule kila mwanafunzi ana gari. Ila mimi nimelelewa kimaadili sana na mama mwajabu.... kiasi kwamba hua mimi sinaga makuu kama dada yangu zaituni.... kwani dada yangu nae ana gari la kuendea shule ila mimi nimekataaa kutembelea gari.. na pia hata simu pia sina maana naona haina faida kwangu
Basi nilifika shjleni kwetu kisha moja kwa moja nikaripoti ofisini ili nijulikane kua nimechelewa shule
JE? WEWE ULISHAWAHI KUCHELEWA SHULE NA UKAENDA KUJISHTAKI OFISINI???? HEEEEE KAMA HUJARUKA UKUTA NA KUINGIA CLASS,
"asalam aleykhum?"
"waalekh msalam vp sheby mbona leo umechelewa shule?"
"nisamee mwalimu"
"najua kua sio kosa lako na hunaga tabia hii ya kuchelewa hivyo nenda tu darasani"
Shuleni kwetu sisi hua tunavaa sale au uniform za kiislam ( panjabi ) na kwa wanawake wanavaa sale za ( hijabu na ushungi juu ) Kiukweli niliingia darasani. afu shuleni kwetu mimi sijawahigi kua mtu wa 3 toka nianze shule. yaani ni nashikaga nafasi ya pili au ya kwanza. Hua walimu wananipena sana hapo shuleni maana mimi hua sina makuu juu ya utajiri wetu. na nina heshma na upole wa hali ya juu kuliko mtu yeyote yule.....
Basi kama kawaida yangu hua mwalimu akichelewa kuingia darasani hua mimi napitaga ubaoni pale na kuanza kukumbushiana tulioyasoma jana.... shuleni kwetu kuna wanafunzi wa kike ambao hawajafunzwa wakafunzika hivyo hua saa zingine wananisumbua sana kua na mahusiano nao...... ila kwakua mimi mwenyewe nimelelewa kimaadili zaidi hivyo watu kama hao kwangu ni bure tu.
Ilifika mida ya saa 10 hivi jioni ambao ni muda wa kukwea school bus.. lakini leo sitopanda bus kwani nilikua na kibaskeli changu nilichokuja nacho...
Sasa nikiwa nipo njiani kuelekea nyumbani mara nikaskia honi kwa nyuma... nikasogea pembeni ili apite sasa nasikia bado tu anapiga honi.. ikabidi nigeuke nimuangalie ni nani anaepiga makele huyo?.....
Aaaagggyyyyy aseee kumbe alikua ni dada yangu zaituni. Aisee ana masifa hayo, Eti kanipitia tuende wote nyumbani yaani katoka koote huko hadi huku kisa tu aje anichukue....
"we sheby twende basi"
Aliniambia hivyo huku akifungua kioo. Sasa alipofungua kioo niliona kajaza marafiki zake wengi hao duuuu. afu ni wazuri ile mbaya Na hao pia wana magari yao ila hua wanapenda kupanga siku watembelee gari ya nani kati yao...
Sasa wale wanafunzi wenzake wakaanza kumuuliza zaituni
"mmmh zai yule ndio nani tena?? au ndio shemu wetu?"
Dada angu aliwageukia kwa hasira
"nyie tueshimianeni bwana"
"mmhh sasa tusikuulize je? tukipita nae je? utatulaumu?"
"bwana nyie yule ni mdogo wangu"
"mmhh zai muongo sema kweli ni mdogo wako?"
"ndio"
"khaaa una mkaka hensamu hadi raha"
"jesca? tafadhali sana punguza mdomo wako"
"mmhh sasa tusimsifie kaka yako?"
"aaahh twendeni bhana kwanza mwenyewe hataki"
"ah ah bwana zai kua mpole... hebu toa loku basi hata nikampe mkono wangu"
Je? Ni nini kitaendelea?
Pres LIKE kesho ije mpya
0 Comment to "SECONDARY SCHOOL Sehemu Ya 1"
Post a Comment