SEKRETARI WA KIUME
Sehemu Ya 12
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/
Ilipoishia Jana...........
MWANAUME MASHINE
"kwani kuna nini manangu"
"mpigie sasa hivi utampoteza mwanao yupo kwenye hatari"
Aliongea nailah tena alikuwa akilia sana, yaani roho inamuuma na anajuta kumfukuza kazi... Mana kaja kuingia pabaya...
"sawa hebu kata simu"
Sasa mama JAFARI nae presha kwa kuskia mtoto wake yupo kwenye hatari....
"boy, njoo uchukue palipo yako"
Shantel alimuita jafari kule kwenye gari,... Madam nailah haamini kama jafari anaingia kwenye gari, sasa madam anajua kuwa jafari ndio anaingia wanaondoka.... Nailah alishuka kwenye gari ili kwenda kumzuia jafari asiondoke... Lakini sasa ile anavuka tu barabara,.. Ghafla kuna gari iliachiwa huko na spidi kali,.na madam alikuwa anavuka barabara, Maskini madam alibaki tu kuduaa hapo barabarani, kukimbia kashindwa, kabaki kusimama katikati ya barabara.... Iliskika tu sauti ya kilio
"uuuuuuwiiiiiiiiiii"
ENDELEA......
Siku ya balaa ni ya balaa tu hata iweje, Madam nailah bado anataka jafari awe mfanyakazi wake, kwani kama mi mapenzi kaenda kufanya mwenyewe, hivyo hakukuwa na sababu kubwa ya kumfukuza jafari,.. Lakini madam akiwa tayari keshamsamehe jafari arudi kazini, lakini jafari anakutana na kazi nyingine mpyaa, afu ina mshahara mnono...
Lakini kazi alioipata inasemekana sio kazi ambayo ataifanya, bali atapelekwa sehemu nyingine,... Sasa wakati jafari anakwenda kuchukua malipo yake ya kujaza upepo,. Madam nailah akajua jafari ndio anapakiwa na kuondoka,... Saa ngapi nailah hajatoka katika gari yake ili kwenda kumzuia jafari asiondoke na kama ni kazini arudi,.. Lakini sasa ile anafika katikati ya barabara, kuna gari iliachiwa kwa spidi kali,... Madam alipiga tu kelele
"uuuuuuwiiiiiiiiiii"
Wakati huo kajifunika na mikono,... Ile anakuja kufumbua, anaona gari ipo miguuni mwake, yaani imesimamia kwenye miguuu... Imebaki kiduchu tu agongwe...
"we dada vipi wewe... Una kichaa nini"
Aliongea dereva wa gari hio ambayo ilitaka kumgonga nailah, na nailah ni kweli ana makosa mana kavuka bila kuangalia popote,..
"samahanini jamani, nilikuwa na mawazo tu"
Nailah alijitambua, lakini nailah tofauti na sehemu alipozoea hua anakuwa mpole kuliko mahali alipo zoea...
"sasa kama unge gongwa je ingekuwaje sasa"
"Samahani kaka.... Niwie radhi tafadhali"
"watu wengine mnataka tuishie jela tu.. Jiangalie bwana"
Aliongea yule jamaa huku akiondoka na gari yake,... Sasa madam ile kugeuka kwa waziba pancha, Shantel alisha ondoka zake, lakini jafari yupo.. Hapo madam akapumua kidogo..hakutaka hata kumfuata aliwasha gari yake na kuondoka,... Mara jafari ndio anapigiwa simu na mama yake
"hallo mama"
"we jafari mwanangu upo wapi sasa hivi"
"mama nipo kwa broo hapa kijiweni"
"sasa mbona unachelewa baba.. Hebu rudi"
"sawa mama... Hapa ndio tunaingiza vitu ndani"
Aliongea jafari mana wanafunga kazi kwa kua usiku umeingia,..
"hebu wahi nyumbani"
"sawa nakuja sasa hivi"
Basi jafari aliendelea kuingiza vitu ndani,.. Baada ya hapo akakatiwa elfu kumi na kaka yake wa mtaani,
"daahh, ahsante sana broo... Hapa inanisukuma kabisa hii"
Aliongea jafari huku akiiweka elfu kumi yake mfukoni
"we Usijali, uwe unakuja tuziokote taratibu dogo langu"
"poa broo"
Basi yeye na kaka yake kila mmoja njia yake, jafari kwao na jamaa nae kwake..
Huku kwa nailah,.. Yaani nailah hata kula hali... Sasa hapa ndio tunajiuliza nailah na jafari kuna nini? Mbona anamuwaza sana jafari, tena kichwa kinamuuma sana pale anapoona jafari anatakwa kimapenzi.. Na anamjua Shantel ni mwanamama anaemiliki wasichana wasiopungua mia moja, na wote anawashughulisha na maswala ya ngono,.... Nailah hakulala kabisa japo kamuona jafari kaachwa na Shantel
Sasa huku kwa akina jafari baada ya jafari kufika nyumbani,... Mama alikuwa mkali sana
"sasa nitakukataza hata kijiweni usiende"
Aliongea mama huku jafari akikaa katika kiti
"kwanini sasa mama"
"saa mbili hiii... Na ulikuwa kwenye hatari gani"
Aliongea mama, huku jafari akishangaa kuambiwa alikua kwenye hatari gani
"hatari??... Hatari gani"
"mbona boss wako kaniambia ulikuwa kwenye hatari"
"yeye aliniona wapi na uongo wake"
"wewe usimwambie dada yako muongo,... Yule ni boss wako"
"alikua boss wangu, sasa sio boss wangu mama"
Aliongea jafari huku asijue kuwa nailah kumsamehe na arudi kazini
"kwanza unatakiwa kuwa na furaha"
Aliongea mama yake jafari uku jafari akimwambia kuwa
"hata wewe unatakiwa kuwa na furaha mama angu"
Sasa mama anajua labda jafari anajua kuwa keshasamehewa kurudi kazini,..
"sasa ole wako uchezee kazi tena"
Sasa mama alimwambia hivyo kwa kutegemea kuwa jafari kufahamu kurudi kwake kazini
"sasa mama? Bado sijakwambia afu unasema ole wangu niharibu... Mimi mama nina nyota mimi wewe"
Aliongea jafari huku mama akisema
"hio nyota yako bila mimi ingekuepo"
Mama Aliongea hivyo huku jafari akisema
"afu ni kweli... We ndio kila kitu bwana... Sasa mama njaa ujue"
"chukua kwenye hotpot hapo"
Aliongea mama yake jafari, lakini mpaka hapo hajui jafari ana furaha ya kazi gani, ila mama anajua jafari ana furaha ya kirudishwa kazini, kumbe jafari kapata kazi mpya...
Kesho yake jafari katola asubuhi kama kawaida yake, na mama anajua mtoto wake anakwenda kazini kwa nailah, lakini sivyo.... Jafari alishapewa namba za simu za Shantel, na pia kapewa maelekezo ofisini kwake... Hivyo hapo alikuwa anakwenda ofisini kwa Shantel...
Huku kwa madam nailah, anaingia ofisini, kitu cha kwanza kumuuliza jafari...
"Aisha"
"yes boss"
"jafari yuko wapi"
"mmmhy boss, jana si ulimfukuza"
"tayari nimesha msamehe"
"hajafika bado"
"saa tatu kasoro hii"
"ndio"
Nailah aliingia ofisini kwake lakini akili haitulii, yaani sijui yeye na jafari kuna nini, hata aisha anashindwa kuelewa jafari na nailah kuna nini kati yao, mana kama vile kuna kaupendo ka kisiri siri...
"hallo mama, Shikamoo"
Nailah alipiga simu kwa mama yake jafari,
"Marahaba mama habari ya kazi"
"salama tu... Aah Samahani mama, iv jafari jana ulimwambia kuwa arudi kazini"
Nailah aliuliza hilo huku mama akijibu
"jana sijamwambia lakini alionekana kujua kabla sijamwambia... Kwahio nikajua tayari ulishampa taarifa... Kwani hajafika"
"hayupo huku kazini"
"huyu mtoto amekuwaje tena jamani"
"ok.. Ila hakuna shida... Niachie mimi hio kazi"
Madam Aliongea hivyo mana anajua fika jafari kaenda kwa Shantel...
"sawa mama"
Na ni kweli huku kwa Shantel na jafari wapo njiani,... Kuelekea kwenye danguro la Shantel... Lakini jafari hajui mana ndio kwanza kapata kazi leo, hivyo anaambiwa tu kata pale, kata kule,... Hapo wanaelekea kwenye danguro
Wakati huo madam nailah nae ndio anatoka, mana anamjua Shantel ndio mwanadada anaeharibu watoto wa kile hapo mjini.. Yaani haswa wale wanaofeli kidato cha nne kwenda cha tano,... Anawarubuni kwa pesa nyingi sana kumbe anakwenda kuwauza,.. Kwenye danguro lake...
Shantel alitoa sauti kwa mlinzi wa geti hilo
"hana shida, tuache tuingie"
Aliongea Shantel baada ya mlinzi kuzuia gari hio, japo boss yupo ndani lakini kwakua alikuwa na mtu asiejulikana Haruhusiwi kuingia bila ruksa yake,.. Mana mambo yanayofanyika huko ndani ni hatari, na hata serikali haijui kitu.. Basi waliingia mpaka kwenye parking za magari...
Sasa ile wanaingia tu na nailah nae huyo,... Lakini hajui kama jafari keshaingia hapa, sasa jiulize nailah kapajuaje.... Kampuni ya akina nailah inahusika na usafirishaji wa bizigo na pia binadamu... Yaani wana mabasi yaendayo mikoani, na pia wana malori ya mizigo.... Sasa basi lao moja lilikodishwa na Shantel kwenda kanda ya ziwa... Yaani maeneo ya Mwanza, Singida, Shinyanga huko.. Na kwingineko.... Shantel alikwenda kanda ya ziwa kutafuta mabinti kwa ajili ya biashara yake, wakifika huko wana wadanganya hata wazazi wa mabinti hao kuwa mjini kuna kampuni mpya imefunguliwa, hivyo inahitaji wafanyakazi,.. Sasa wazazi wakiachiwa kitu kidogo wanajua kweli kuna kazi.. Basi wanaachia watoto wao,... Sasa basi liliotumika kubeba wasichana hao ni moja ya mabasi ya kampuni ya akina nailah, kwahio hata siku anafuatilia ishu ya malipo ya usafirishaji wa wasichana hao, alikuja hapa.. Mana ilikuwa ni pesa ndefu haikufaa kutuma mtu, japo malipo ni kwa cheki lakini nailah alifuata mwenyewe.... Na ndio maana hata leo haikuwa kazi kuja mpaka hapo,... Mana alishawahi kuja kufuatilia malipo ya usafirishaji wa hao wasichana....
Sasa madam pamoja na kujulikana na mlinzi lakini bado hakupewa ruksa ya kuingia,.. Lakini akaambiwa kuwa boss atatoka muda sio mrefu...
"kaingia na kijana huku ndani"
"ndio"
Madam kujibiwa hivyo alitamani hata kupaa mpaka huko ndani... Basi alirudi nyuma na kupaki gari yake mahali,... Sasa hawa walinzi hua wana shift,.. Sasa wa mchana ndio anaingia na wa usiku anatoka.. Nailah hakumuacha yule mlinzi.. Kampigia honi mlinzi akaja...
"Samahani nikupe lift"
Madam alimwambia mlinzi huyo kuwa ampe lift, na ana maana yake kumwambia hivyo... Kweli mlinzi kuona ni tajiri afu mtoto mzuri, kaingia kweli kisha gari ikaondoka..
"vipi umepata supu wewe"
Aliongea madam nailah, mtoto mzuri mwenye asili kama ya shombe shombe hivi, umbo lake ndio usiseme, yaani kakaa kibantu bantu... Mwanaume nani asivunje shingo kwa nailah???.... Lakini kutokana na staili yake ya ukali,.. Hakuna mwanaume anamsogelea hata mmoja...
"bado dada, si ndio natoka shifti hivi"
"ooohhh wacha nikupeleke novo hotel ukapate supu sawa"
NOVO (NOVEL) HOTEL ni hoteli fulani kubwa jijini Arusha japo zipo kubwa yake lakini hio ilisifika sana.. Sasa mlinzi hajawahi hata kupata bahati ya kulinda hata nje, leo anapata bahati ya kwenda kula supu kabisa
"sawa dada"
Kama unavyojua walinzi hua wanajiona wao ndio watu wa mwisho kupendwa,.. Kakubali vizuri mpaka ndani
Mlinzi kapigwa supu safi, kapigwa chai nzito... Kisha madam akaanza kumuuliza
"Samahani... Nataka unipe imfomeshen ya pale ndani"
Mlinzi kuskia hivyo hata kunywa supu aliacha,...
"wewe ni askari"
"sina maana hio"
"sasa nini shida"
"ni binafsi tu... Kwasababu kijana alie Ingia pale, ni mdogo wangu"
Mlinzi kuskia kijana alie ingia pale ni mdogo wake, alishtuka sana lakini pia hakutaka kuonyesha ushirikiano, mara nailah akatoa kitita cha pesa
"niambie mwanzo mwisho... Watu wanaingiaje pale"
Mlinzi kuona hela, na ugumu huu wa maisha... Ilibidi akae kwenye kiti vizuri... Kumbe ni imfomeshen tu, aaahh mlinzi kapokea hela kisha kaanza kutapika ukweli wa lile jengo
"bwanadada pale mahali ni pa kishetani.... Kwa sasa wasichana mjini hakuna wa kuwarubuni mpaka inafikia hatua wanakwenda mikoani kuwarubuni wale wasiojua lolote... Wakija huku wanaingizwa kwenye biashara ya kuuzwa... Lakini hapo ndani, kuna makundi mawili ya wasichana.... Kuna kundi la kuuzwa... Halafu kuna kundi la waigizaji"
Nailah kuskia kuna kundi la waigizaji akataka kujua zaidi... Mana alisikiaga tu
"hilo kundi la waigizaji ni lipi"
Aliuliza madam nailah huku mlinzi akijiachia na ukweli wote
"pale kuna sehemu mbili... Ila jengo unaona ni moja lakini yapo mawili... Jengo moja ni la Wasichana wanaouzwa, hao hawaruhusiwi kutoka nje, na wanaokuja pale sio wanaume lala hoi... Pale wanakuja matajiri watu na pesa zao.. Ndio wanakuja kununua wasichana"
"ok ngoja kwanza... Sasa hao matajiri wakinunua wanatoka nao au"
Aliuliza nailah
"hapana... Humo humo kuna hoteli ya kifahari, hivyo wakinunua, wanapewa na vyumb bure... Ila msichana kamnunua wa usiku kucha"
"ok na hilo kundi la kuigiza nalo likoje hilo"
Nailah alizidi kuuliza zaidi ili kujua vizuri
"sasa hili kundi la kuigiza hili... Wasichana wanaoletwa kwa ajili ya kuigiza hua wanakuwa ni wazuri mno na wenye maumbo makubwa... Wao kazi yao ni kuigiza video za ngono... Na hao pia hawaruhusiwi kutoka, kwa kuepusha kwenda kuzoa ugonjwa huko nje"
"kwahio hapo ndani hakuna ugonjwa"
"kwa wale wa kuigiza, hua hakuna ugonjwa mana kila anaeletwa hupimwa magonjwa yote kisha anaingia kazini,... Na akikutwa na magonjwa Haruhusiwi kuingia,... Mana kwenye kitengo cha kuigiza kuna madaktari wa kuwafanyia usafi na kuwapima afya zao kila siku.. Na wanalipwa vizuri ila magonjwa ndio hawana... Ila hao wa kundi la kujiuza huko... Kiukweli sijui mana wanaume wao wanatoka nje"
"enheee, sasa je hao wa kuigiza wanaume wa kuigiza nao wanatokea wapi kama sio hao hao wa nje"
Madam alikuwa na maswali mpaka anamchosha mlinzi wa watu
"kwa wanaume wa kuigiza hua anawaleta boss mwenyewe..."
"hebu ngoja kwanza.... Anawaleta leta vipi sasa, au nao wanaletwa na mabasi"
"hapana... Hao anawaleta yeye mmoja mmoja,... Na wote anaowaleta hua anawapa kazi ya udereva,... Lakini kazi ile anampa ili ampime kama ana nguvu za kiume vizuri... Na ili ajue kuwa ana nguvu za kiume ni lazima atembee nae yeye mwenyewe kwanza... Afu ndio anaingia nae kwenye kitendo cha kuigiza... Na hapo lazima awe keshapimwa magonjwa pia... Hivyo kundi la waigizaji ni salama kuliko la wauzwaji"
Mlinzi Aliongea yote lakini madam akawa kama bado hajaelewa
"lakini sasa huoni wanaume wa kundi la kuigiza watakuwa ni wengi sana"
Aliuliza madam mwenye maswali kama polisi
"hapana... Hua vijana wale wanafanyishwa kazi ile kila siku... Na wanapoishiwa nguvu kuna mafuta hupakwa kwenye viungo vyao... Ili waweze kufanya kazi ile kila siku.... Sasa inafikia hatua hata kijana akipakwa yale mafuta, bado anafanya kazi kwa kusua sua.. Sasa hapo boss anamtoa nje, mana hawezi kazi tena... Kwahio inakuwa ni hasala kwa watoto wa kiume"
Madam kuskia hivyo, tumbo lilimkata, chaaaaa
"sasa... Uuuwiii...sasa...kwa mfano huyu alieingia leo, hatoki tena"
Madam aliuliza huku akilia, yaani sijui kwanini anamsaidia jafari
"hapana... Huyu alieingia nae sasa hivi, hawezi kusajiliwa haraka haraka.. Ni mpaka atembee na bosa kwanza ajue uwezo wake... Kisha ndio anaenda kumsajiri, na hata hapo huyo alie ingia hawezi jua ndani kunaendelea nini,... Mana hatopelekwa kwenye kumbi za aina hio, bali ataishia ofisini tu.."
"iiiiiiiiiii.... Uuuiiii.. Basi baba, ahsante kwa ushirikiano wako"
Madam aliondoka zake na mlinzi hakubaki hapo, ila keshajipatia kitita chake saafi kabisa,..
Sasa huku danguro kwa Shantel, alikuwa akiongea na meneja msimamizi wa kazi zake... Hususan kwa upande wa waigizaji... Na alikuwa ni mwanamke kama ilivyo kawaida ya wasimamizi wa waigizaji wa ngono, hua wanakuaga ni wanawake...
"naona kuna boy kwenye gari, vipi... Ni mwigizaji mpya nini"
Aliuliza meneja huyo mwanamama
"yes, but, lazima nikajue uwezo wake Kwanza.."
"mi naona ungefanya hima... Mana vijana wetu wa kiume, Kiukweli wote wameshakuwa dhaifu,.. Wanapanda mara moja tu afu basi, ni mpaka kesho"
"ok jana mlirekodi video ngapi"
"tatu tu"
"khaaaa... Tatu... Kivipi ziwe tatu"
"vijana wamechoka..."
"wapakeni mafuta"
"yaani tunawapaka sana tu boss, lakini bado wako dhaifu"
"aiseee... Yule tajiri wa Uingereza kanitumia Email kuwa anataka mzigo.. Na anataka muvi kama 50 hivi zenye masaa matatu matatu"
"heeeeee boss, wanaume waliopo hapa, hakuna anaeweza kufikisha huo muda yeye peke yake... Labda wasaidiane"
"basi ngoja... Nikampime huyu... Afu nijue uwezo wake... Nitamleta jioni... Sasa andaa ile kamera inayo rekodi 4K"
Aliongea Shantel huku akitoka na kwenda kupanda gari, kweli mpaka hapo jafari hajui hilo jengo linahusika na nini... Na mlinzi alisema mtoto wa kiume wa kuigiza hua anasajiriwa baada ya wiki... Sasa imeonekana vijana wa kuigiza hawana nguvu, hivyo jafari leo jioni atatakiwa kuingia mzigoni,... Na hua hawakatai kwasababu wanapewa pesa nyingi, na pia anaahidiwa kulipwa pesa nyingi kila wiki kama vile mchezaji wa mpila... Unakuta unaambiwa kwa wiki utalipwa milioni mbili... Kama ni wewe utaacha kweli??
Sasa wakati huo madam anakuja huku danguroni, na Shantel nae anatoka kwenda hospitali kumpima jafari mana wakiume hua hawapimwi humo ndani, wanapimiwa hospitalini, na akitoka kumpima, wanapitia hotelini,.. Kwa uzuri wa Shantel hakuna mwanaume ataambiwa alale na Shantel akatae... Sasa madam anakuja kwa Shantel, na Shantel nae anatoka.... Sasa sijui kama watakutana
GHARAMA YANGU NI SHARE 200 TU,
ZITAKAPOFIKA TU, NAENDELEZA...
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/
STORI ZANGU ZOTE HIZI HAPA....
(1).KIJAKAZI WA KIUME
(2).MLINZI WA GETI
(3).DEREVA TOYO
(4).MTOTO WA HAYATI
(5).ONE DAY YES
(6).SECONDARY SCHOOL
(7).FUNDI CHEREHANI
(8).MWIGIZAJI BALAYA
(9).THE DOM
(10).THE ISLAMIC WIFE
(11).MKE JEURI
(12).YOUNG PASTOR
KUZISOMA ZOTE, BONYEZA HAPA
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/
AU.... NICHEKI KUPITIA NAMBA +255714419487 WhatsApp
Utazipata Zote Mpaka Mwisho Kwa Simu No: +255714419487 WhatsApp, Au, Like Page Yetu Ya Facebook Kwa Kubonyeza Hapa Chini ili Usipitwe
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/
tAfBoy {.Tanzania's Frugal Boy..}
0 Comment to "SEKRETARI WA KIUME Sehemu Ya 12"
Post a Comment