Monday, November 27, 2017

DEREVA TOYO Sehemu Ya 1

DEREVA TOYO

Sehemu Ya  1

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No.... +255714419487 WhatsApp

Inapoanzia Rasmi..... Anza Sasa

DEREVA TOYO AU KWA KINGEREZA TUNAITA ( TOYO DRIVER )
DEREVA TOYO HUYU NI KIJANA MDOGO ALIEJIAJIRI KUTOKANA NA USAFIRI HUO ( TOYO ) MBALI NA UDEREVA WA HIO TOYO... BADO ANA AJIRA YAKE YA MKONONI..... NI AJIRA YA UPIGAJI PICHA... NA HII ALIANZA NAYO KABLA YA TOYO KIJANA HUYU ALILAZIMIKA KUWA DEREVA TOYO KWA SABABU ZA KIMAISHA KUMUENDEA KOMBO... HIVYO AKAONA TOYO HUENDA IKAMPA CHAKULA CHA KILA SIKU... LAKINI TOYO HIO HIO NDIO ILIOKUA IKIMPELEKA PABAYA.... KWANI KIJANA HUYO ALIKUA NI KIJANA WA TOFAUTI SANA..,..
KWANI ALIKUA AKIIINGIZA PESA NYINGI SANA KWA NJIA YA TOYO... MPAKA MADEREVA WENZAKE WANASHANGAA NI KWANINI MWENZAO ANAPATA PESA NYINGI KIASI HIKI..... KWASABABU SEHEMU AMBAYO AKIMPELEKA MTEJA WAKE ALIPASWA ALIPWE 3000 AU 2000 LAKINI ANALIPWA 10000 ( ELFU KUMI ) MPAKA WENZAKE WAKAJENGA WIVU JUU YAKE NA KUMTIMUA KIJIWENI KWAO..... LAKINI SWALI LINAKUJA HIVI..... JE? NI KWANINI KIJANA HUYO ANAPATA PESA ZAIDI KULIKO WENZIE ALIOWAKUTA..... NA LICHA YA TOYO... PIA KUNA HII KAZI YAKE YA UPIGAJI PICHA

YAANI NI KAMA HAWA WAPIGA PICHA WA MTAANI AMBA HUA MNAPENDA KUWAITA SIKU ZA SIKUKUU ILI KUPIGA PICHA ZA UKUMBUSHO

KWA SISI HUKU ARUSHA HUA TUNAWAITA  "MCHAGAA PICHA"  NA HATA KAMA SIO MCHAGA ILA TUTALAZIMIKA TU KUMUITA HIVYO

SASA HUYU KIJANA YEYE KAZIDI MNO KATIKA FANI HIII YA UPIGAJI PICHA.. KWANI KWA KAWAIDA YA PICHA NI SHILINGI ELFU MOJA TU... ILA YEYE ANAPEWA LAKI MOJA KWA KUMPIGA PICHA MTU MMOJA.. NA PICHA ZAKE HAKUNA MTU ANAEWEZA KUZIONA KUA HUA ANAPIGAGA PICHA ZA DIZAINI GANI

JE? UNAJUA NI KWANINI KIJANA HUYO ANALIPWA KIWAONGO TOFAUTI NA WENZIE?????

ILI KUJUA YOTE ANAYOYAFANYA MPAKA KIWANGO CHA PESA KUONGEZEKA KULIKO WOTE NI NINI???

KWA MARA YA KWANZA NAMTAMBULISHA KWENU KWA JINA LAKE TUUUU

ANAITWA..... James AU UKIPENDA MUITE.... Jimi..... KWA KIFUPI YANI...

JE? KAZI ANAYOFANYA JAMES NI YA KICHUMA ULETE AU NI JUHUDI ZA KAZI????

MIMI SIJUI ILA FATANA NAMI ILI KUJUA MKASA MZIMA WA JAMES

TWENDE KAZIIIIIIIIIIIIIIIIIII




ENDELEAAAA.......

Leo nilikua mtaani kwetu sina ramani wala nini. Na bado naishi na wazazi wangu wote.
Kama unavyojua tena ujana huu

Basi mtoto wa kiume nilitoka pale kijiweni na kuelekea nyumbani mida ya mchana ili kupata chakula cha shikamoo....

MIMI HUA NAISHI USWAZI KABISA YAANI SEHEMU KUNAKO NYUMBA ZA UDONGO NYINGI... MZUNGUKO WA BIASHARA ZA KISWAZI KAMA VILE MIGUU YA KUKU AU SAMAKI AU MIHOGO.. NA KADHALIKA.. TENA ISTOSHE KITAA CHETU KINA VICHOCHORO HIVYO DUUU KWELI NI USWAZI....

Basi mtoto wa kiume nilifika hadi nyumbani tena nilimkuta hadi baba yupo
Maana siku hio ilikua ni siku ya juma pili hivyo wazazi wangu wapo...
"shkamoo mzee?... shkamoo mama?"
"marahaba.... unatoka wapi saa hizi na jua lote hili mwanangu?"
Alikua ni mama angu huo MWAJABU
"mamaa si unajua mishe mishe hizi"
"mishe mishe gani mwanangu wewe... eeh? hebu ona vijana wenzio umekua nao lakini sasa hivi wana kazi za maana na vyumba wamepangisha"
"asa mama mbona unanisemaa?"
"sio nakusema mwanangu ila umezidi uvivu"
"kwani si nina kazi mama"
"loooo kazi gani? hio ya kupiga picha? kazi gani hata faida huna"
"aah nitapata tu"
"utapata tu hadi lini? baba ako anataka kukutafutia kazi afu we unaruka ruka tuu"

Mara mzee kadakia juu kwa juu

"hili liende gereji hili... maana likikaa hapa litakuja kua likibaka hili"
"wewe baba JIMI usimuambie mtoto hivyo bwana"
"wapi bwana Afu wewe ndio unamdekeza wewe"
Mzee alianza maneno ya hapa na pale huku akiwa ana hasira nyingi mno..
Basi hio ni kawaida ya wazazi hata kwenu pia naamini yapo.. kua mama ndio chanzo cha mtoto kuwa mwehu na jeuri au asiesikia....
Basi nilikula cha mchana pale kisha nikaenda misele ya hapa na pale




Na sasa ni usiku mida ya saa mbili kamili hivi
"sasa baba jimi? tumfanyaje mwenetu? maana hana kazi huyu"
"wacha niende nae gereji huyu"
"mbona unamng'ang'anizia tu huko? kwani kazi zipo gereji tu?"
"sasa anaelimu gani? si kakimbia shule huyu? mimi nifanyeje?"
"tuangalie njia nyingine bwana.... Eti mwanangu kwani unataka kazi gani?"
"labda toyo"
"umeona sasa mwanao alivyo mjinga?? yaani anaona kabisa toyo zinaua lakini linaenda tu"
"sasa baba mbona kaka ni dereva toyo lakini hamumkatazi?"
"yeye pia alikua kiburi kama wewe... na tulimwambia lakini hakusikia"
"sawa ila si nitakua makini mzee"
"si unawaona wanao wataka wote wafe na toyo?"
"lakini we mpe tu jamani"

"yaani mama jimi unaniuzi wewe... kwanini kila kitu mpe?"
"sasa kama ni gereji hataki utaenda kunivunjia mwanangu mikono bure... na mwenyewe ndio wa mwisho huyu"
"kwahio sisi tulioko huko tuna miili ya chuma si ndio?"
"aaa sijamaanisha hivyo mimi"
Baba akaniambia "sasa sikia james.... wiki ijayo nitakwenda kwa mjomba wako ili anipe hio toyo moja... maana aliniambia zipo ndani na hazina mtu"
nikamjibu "sawa nitasubiria tu"
Basi maongezi yaliisha na usiku ulipita...

na sasa ni asubuhi mida ya saa 4 hivi
"we jimi?"
"naam mama?"
"njoo unywe chai"
Nilienda kunywa chai ya shikamoo
baba alisema
"hili toto siku moja liache na njaa ili lipate akili"
mama akamjibu "sasa utakua unamkomoa au unamtesa jamani?"
baba akamwambia "mi nakwambia kama sio wewe asingekula milo mitatu huyu"
"heee kisa cha kumtesa mtoto?"

Mara nikaitwa huko nje
"jimi?"
"yes nani ananiita?"
"rehema"
"aaahh nisubiri kidogo"
"poa"

baba alisema "umeona? yaani linapenda wanawake hili toto hili"
"mzee mbona ivyo majungu mengi"
"unaona mwanao ananitusi huyu."
"jamani baba jimi.. sasa kakutusi nini hapo?"
"wee huezi ona maana kila neno lake kwako ni tamuuuu.... na ndio maana nakuambia unamdekeza"

"mama? mi naenda maana mzee keshaanza maneno yake"
"neenda tena potelea"
"iiiiii baba jimi mbona unamfukuza mtoto?"
"ameshakua huyuu mbona kaka yake kapangisha rumu yake"

Nilitoka zangu nje na kukutana na rehema
"mambo?"
"poa tu vp mbona wazazi wako wanagomba au ni mimi nini kuja hapa?"
"aaa wala tu .... hawa wana swaga zao"
"sasa kuna sendof jioni hivyo kama vipi ukapige picha kule gaden rozi"
"ndio huko sendof inakofanyika?"
"ndio"
"ok poa"
"ila usiniangushe na pamba.... maana nikifika pale nitajitangazia kua ni kaka angu"
"haaaa wewe si unanijua milipuko yangu?"
"najua vizuri ila ya leo vunja kabati"

LIKE 50 TU

NIIENDELEZE SASA HIVI


Sambaza Upendo Na Usiwe Kilaza

JAMANI STORI ITAKUA FUPI FUPI KUTOKANA NA UTUNGAJI WENYEWE ULIVYOPANGWA.... HIVYO MSILALAME KUA NI FUPI KWANI NI TATIZO LA MTUNZI

Share this

0 Comment to "DEREVA TOYO Sehemu Ya 1"

Post a Comment