Sehemu Ya 1
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Inapoanziaaaa→↓↓↓
ONE DAY YES ni msemo unaotafsiriwa kua IPO SIKU YATAKWISHA kwa maaa ya kwamba mtu huyo anaesema hivyo yupo katika hali ngumu ya kimaisha au misuko suko ya hapa na pale.
Msemo huo ni msemo unaotaamkwa na mtu mwenye shida ya kimaisha hivyo kila siku lazima mtu huyo aseme ONE DAY YES kwa maana ya kwamba IPO SIKU NA YEYE ATATUSUA kama wenzake,
Kijana mdogo huyu alieitwa RASHIDI TUNDI KINGAZI MWENYE UMRI WA MIA 21 alizaliwa katika kijiji kimoja kilichopo mkoani TANGA kiitwacho PANGANI KIKOKWE ni kijijini sana huko, Kijana huyo alikua ni mtoto wa mwisho katika familia yenye watoto wanne (4)
WA KWANZA NI KAKA YAKE ALIOPO MJINI ARUSHA NA ANA PESA KIASI FULANI LAKINI HATUUJUI MSAADA WAKE KATIKA FAMILIA....
NA WA PILI NI KAKA YAKE PIA, AMBAE WANAISHI WOTE KIJIJINI KWA KULIMA MAZAO KWA PAMOJA ILI KUMSOMESHA DADA YAO...
NA WA TATU NI DADA YAKE NA RASHIDI AMBAE KWA SASA BADO ANAENDELEA NA ELIMU YAKE YA CHUO HUKO DAR, KATIKA CHUO KIMOJA KIITWACHO mlimani city KWA UDHAMINI WA SERIKALI NDIO MAANA KAENDELEA MPAKA HUKO ILA BILA HIVYO ANGEISHIAGA DARASA LA SABA KAMA MDOGO WAKE RASHIDI......
NA MTOTO WA NNE NA WA MWISHO NDIO HUYO RASHIDI SASA AMBAE NDIO ANATUELEZEA YALIOMKUTA MPAKA SASA HANA NDUGU WALA NINI, ILA KIJANA RASHIDI NA NDUGU YAKE JUMA WAMEOA WOTE.... ILA HATUJUI HUYO WA MJINI
LAKINI CHA AJABU KIJANA RASHIDI ANAKUJA KUA TAJIRI MKUBWA KULIKO....JE? ATAUPATAJE HUO UTAJIRI???
........ HEBU ANZA RASMII KUISOMA HIII ↓↓↓ STORI
~KATIKA STORI ZOTE NILIZOANDIKA HAKUNA NILIOIPENDA KAMA HIII, MAANA INA MAFUNZO JUU YA MTU ANAEKWENDA MJINI~
TWENDE KAZI NA KASTORI KETU
↓↓
Tulikua shambani mimi na kaka yangu juma, tukiwa katika mapumziko ya kupata mihogo ili tuendelee kulima vibarua vya watu, Wakati huo mke wangu na mke wa kaka yangu walienda kutafuta kuni, kwa ajili ya kurudi nazo nyumbani maana ndio wametuletea chochote cha kukazia tumbo....
"unaskia broo?"
"sema?"
"mi nafikiria kwenda mjini kwa broo"
"nini? ivi una akili wewe? nakuuliza una akili wewe?"
"kwanini sasa?"
"yaani unajua kabisa familia yetu yote inatutegemea sisi afu tena unataka uende mjini? unawaza nini mdogo wangu eee?"
"sawa kaka mimi najua kua familia inatutegemea sisi wawili tu, ila tutaendelea kupiga vibarua mpaka lini?"
"mdogo wangu mdogo wanguuu achana na imani potofu, mbona maisha yanaenda tuuu? Hebu fikiria kaka yetu mkubwa alivyotutelekeza tunamsikia tu kwenye maredio akitangazwa kua tajiri wa tanzania nzima lakini sisi ndugu zake tunateseka tuuu"
"sawa mimi sikatai lakini wacha nami nikayajaribu maisha ya mjini"
"mmhh haya ongea na wazazi kwanza lakini"
"nitajaribu..ila wakikataa mi natoroka"
"nini? acha ujinga... utakuja kuachiwa laana bure Omba kwa hekima zote ukubaliwe"
Basi tulikua tukishauriana na kaka yangu, ili nijue nitaondokaje kijijini... basi tuliendelea kulima heka za watu ili tupate chochote cha kutuwezesha kiasflani katika maisha.
Tulilima pale kwa muda na wake zetu walikua wakitusubiria ili tuondoke wote,....
"mama said nenda tu nyumbani si unaona una mtoto mdogo huyo?"
Mke wangu alikua ana mtoto mdogo ambae kazaa na mimi... yaani mtoto wangu mimi
"bwana baba said twendeni bwana"
"hapana, kwani sisi hatutaki kuacha kitu hapa"
Mara broo akaingilia kati na kusema
"aaaaa muache tu kama hataki kwenda"
"hapana bwana kaka ana mtoto mchanga sana huyu"
Kutokana nabkung'ang'ania kwa mke wangu Nilibidi nitulie tu maana kagoma kwenda mwenyewe, Ila hata mke broo nae yupo, hivyo nilimuacha tu......
Basi tuliendelea kulima pale huku tukipiga stori za hapa na pale ili jembe litembee vizuri... na mimi nilikua nalima balaa yaani kwa siku nusu heka inaisha hivi hivi yani..... ila sema tu pesa wanazotulipa ni chache sana hivyo duuu haikidhi mahitaji kabisa,
Basi ilifika mpaka mida ya saa 7 hivi tuliweka majembe begani na kumpigia bosi alietupa kazi.. kisha akatutumia elfu 15 kwenye M-pesa.. ila ni baada ya kumuambia tumemaliza nusu heka yake...
"Yaani broo eti nusu heka tunalipwa elfu 15 kweli????? Eeee mungu seidia tu"
Tulikua tukilalamika juu ya kipato tulichopewa na boss, maana kazi ilikua ni ngumu afu malipo madogo.. basi malalamishi yetu hayakuseidia kitu na wala hayajambadirisha mtu
Muda huo wa saa saba juu ya alama na muda huo jua lilikua likiwaka vibaya mno... hata kijijini kwetu hakuna hata mazao ya maana
Tulikua katika moja ya njia yetu ya kila siku, Na wakati huo mke wangu na mke wa broo walikua mbele wakiwa wamebeba kuni kichwani...
nilimsikitikia sana mke wangu maana ana mtoto wa miezi 6 tu.. yaani mke wangu hata uzazi tu hajala kabisa yaani alibahatika kula kuku mmoja tu, katika uzazi wake na pia hakuna mtu aliemseidia, kwani kipindi hicho mama angu alikua anaumwa. na dada yangu yupo shule dares lam, yaani mimi dio nilikua karibu na mke wangu kwa kumtunza uzazi nini na nini... daah nazani mnajua hivyo tusiliongelee sana....
Mke wangu nampenda sana tena toka alivyonizalia mtoto ndio nilizidi kumpenda zaidi pamoja na saidi wangu
Sasa wakiwa wake zetu wapo mbele na sisi tulikua nyuma.. hio ni baada ya kuvuka korongo moja hivi lenye kupitisha maji machache sana...
Nilichomwa na mwiba mkubwa tu mguuni... maana vijijini kutembea peku sio jambo la kushangaaa
Sasa ikabidi nichuchumae ili niutoe ule mwiba maana damu nyingi zilikua zikitoka,
"nini rashidi? umefanya nini tena?"
Ni broo wangu aliniuliza kihivyo
"ni mwiba tu usjali kaka"
Basi tuliseidiana kutoana na wakati ho nae mke wangu kaja mbio huku akiuliza kuna nini. Alipoona damu zinatoka kwangu ilibaki tu kidogo azimie afu na vile alikua ana mtoto mgogoni sijui ingelikuaje kwakweli....
sasa baada broo wangu kumzuia na kumueka chini... nilimuelezea kilichotokea huku nikijitahidi kusimama... basi niliutoa mwiba ule kisha nikawa najitahidi kusimama... basi tukaanza kupiga hatu za kuelekea nyumbani, Sasa kabla sijamalizia hatu kadhaa niliskia
"vuuuuuuu"
Kwa nyuma yangu, lakini sikuona mtu kabisa
"broo we ndio merusha jiwe huku nyuma?"
"jiwe? saa ngapi nilishika jiwe?"
"au ni wewe shemu nini?"
Nilimuuliza mke wa broo kiutani tu. sasa kabla sijapiga tena hatua niliskia tena ile sauti.. ya mtu kupita kwa spidi nyuma ya mgongo wangu
"Broo tuache masihara bwana mbna mnarusha mawe?"
"nani karusha mawe wewe?"
"ok poa twendeni"
Tulianza safari huku tukipiga stori za hapa na pale
Lakini ghafla niliguswa usogoni mithili ya mtu alienisodoa...
"aiseee broo mbona mi sielewi?"
"nini wewe?"
"nani kanigusa kwa nyuma?"
"sasa mimi nipo mbele nitakugusaje kwa nyuma?"
"eeeehh??"
"Eeenhh eee eee Eeee nini sasa?"
"eeee?"
"nitakutia makonzi rashidi sitaki mchezo"
"eeeee?"
Sasa ilikua naitikia tu eeee bila kujielewa kua ninachokifanya sicho
Ilifikia mahari nimelitupa jembe kisha nikaanza kurudi nyuma tena nikielekea kle korongoni tulipo papita mwanzo
"we chidi unaenda wapi uko?"
Nilikua simsikilizi mtu huku bado nikiwa naitikia eeee kama vile kuna mtu alikua ananiita hivi...
"we chidi twende bhana unaenda wapi huko?"
Mara mke wangu akamuuliza broo
"ana nini yule?"
"mi sijui ndio namuoa sasa hivi"
"sasa si umfatilie jamani shemeji"
"aaaa huyu ana utani sana uyu usikute anatuchezea tu"
"jamani shemeji nenda kamuangalie"
"au anaenda kunywa maji nini?"
"mmhh toka lini akanywa maji ya korongoni?"
"mi sijui kwani si mumeo"
Sasa nilipokua naeda kulikua na korongo kubwa tu...ambalo nikidondokea huko basi na kifo ni huko huko...
Nilifika hadi mwisho wa lile korongo... yaani nikipiga hatua tu basi tena na sitokua mimi tena...
Sasa nilipofika hapo nilishindwa kujua pa kuelekea hivyo.. nilibaki tu nikiwa nimesimama pale
ghafla Kulidondoka jani la mti lakini sio jani kama jani... bali lilikua na ujumbe fulani..
Nililiokota na kulifungua kwa haraka
Heeeeeee nilishangaa kilichoandikwa humo kwenye hicho kijani
Eti kimeandikwa hivi
"usi.................
Gonga like iendeleeeee
0 Comment to "ONE DAY YES Sehemu Ya 1"
Post a Comment