{The Prostitute Actor}
Sehemu Ya 15
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Ilipoishia Jana →↓↓↓↓â†
dakika mbili mbele niliskia naitwa huko chumbani kwa dada yobi, Nilienda kumsikiliza dada wema ananiitia nini, nilipofika nilimkuta kavaa taulo tuu, afu ananiambia nimpe sabuni, huko bafuni, si unajua milango ya alminiamu ilivyo kwa mbaali, nilikua naogopa na kuona aibu, nilichukua sabuni ya kuogea, sasa nikawa nampa huku nikiangalia pembeni, mara katoka kabisa bafuni vile vile na taulo lake,
"ivi wewe nikuulize kitu"
Nilitikisa kichwa kuashiria sitaki na huku nilikua bado nimeangalia pembeni, yaani sikutaka kumuangalia.
"eti sheby, ivi utaweza kuigiza kweli wewe"
"kwani ni lazima tuigize na mataulo"
"sio lazima ila kuna pati utakuta mkeo aba taulo, ina maana utaangalia pembeni katikati ya muvi"
"nitaangalia ndio"
"mjinga wewe, hebu nipe sabuni uko, mtoto wa kiume mno unaogooopa, au unahisi mi ni dada yako eee"
"chukua sabuni niondoke"
Mara ghafla nikaliona taulo limerushwa mbele yangu, Na ndio taulo aliokua kalivaa, sasa kama ndio hili je yeye atakua kabakiwa na nini,
ENDELEA......
Sikutaka kugeuza macho lakini nilijua tulazima awe hana chochote kile, akili yangu iliwaza mambo mengi sana kuhusu jambo hilo, japo kweli napenda lakini nami napaswa kuangalia na hali ya afya yangu, Kiukweli niliitupa sabuni chini na kuondoka bila hata ya kumtazama dada wema, mana alifanya kusudi haswaa ili tu kuniweka katika wakati mgumu,
"sheby,.....sheby...we sheby si ninakuita afu unazidi kwenda tu"
"maliza kuoga kwanza afu uniite"
"yaani we mtoto mjinga sana wewe"
Nilitoka zangu nami nikaelekea bafuni kwangu kuoga, nilipomaliza nilifungulia tv hapo hapo chumbani kwangu nikawa naangalia huku nikishushia na juisi, Wakati huo ndani kwa dada yobi kuna rafiki yake ambae ni wema, na mida hio yatimu saa kumi na mbili hivi jioni....
Ilipofika saa moja, naona mbona haendi nyumbani kwake huyu mtu, ikabidi niingie chumbani huko ili kutazama anafanya nini wakati wote huo, lakini kufika sikukuta mtu... Niliingia bafuni alipokua anaoga
"ooooohhh shit, kaacha kinguo chake huku aisee wanawake bwana daahhh... Sasa hii nguo ya ndani kamuachia nani huku, au huko kwake hakuna kamba ya kuanikia nguo kama hizi,.. Daaa watu wengine wanakusudi jamani mmmhhh haya bwana"
Nilikua najisemea mwenyewe huku nikifunga bafu hilo, mana dada wema alipomaliza kuoga alifua kisha akaianika sehemu spesho humo bafuni, lakini haikupaswa aiache humu mana sio bafu lake, na wala sio kwake
Sasa nilipomuuliza jeni,
"jeni, iv dada wema kaenda wapi"
"mmnhh katoka hapa kwa hasira, nikamfungulia geti huyoo kaondoka zake"
"Eti kaondoka kwa hasira"
"ndio, na sijui kauzishwa na nani"
"mmmhh mi sijui"
Nilisema sijui lakini nahisi mimi ndio niliemuuzi na hata ile nguo atakua kaisahau bahati mbaya tu, mana alikua na hasira kama alivyosema jeni, Nilichokifanya ni kurudi ndani na kuendelea na mambo yangu, ikiwa yaenda mida ya saa 1 kasoro, nilikua nawaza sana kuusiana na kupona kwa dada yobi, Sas nikiwa katika mawazo mengi mara simu yangu iliita, Nilipoangalia jina la mpigaji Alikua ni Sauna.....
"mungu wangu uyu mtoto anataka nini jamani"
Nilijiongelea kimoyomoyo huku nikijiandaa kuipokea simu hio
"haloo bae mambo"
"poa tu,... Jamani sheby ndio nini hivi lakini"
"nini tena sauna"
"yaani wiki ya pili hii nilikua nakutega tu kama utanipigia au hutonipigia, kwanini umekaa kimya ivo lakini"
"baby maisha tu, si unajua utaftaji ulivyo mama angu"
"jamani sheby, mbona unataka kunipa dhambi bure, siku ile nilikupa kiasi gani"
"milioni tano"
"ina maana zimeisha au"
"aahhh Kiukweli sitaki kakudanganya sauna, ukweli ni kwamba mimi nipo Dar es Salaam kwa sasa"
Mara nikaskia mshindo wa kudondoka kwa simu
"pwengele pwengele"
Na hapo hapo simu ikakata, hapo ndipo nikajua kua sauna kadondosha simu, baada ya kumuamnia kua mimi nipo dar kwa sasa,
Nilimpigia tena sauna wa watu maskini ya mungu wee
Lakini simi haikua hewani kwa qakati huo nilipokua napiga,
Mara simu ikaita tena, na alikua ni yeye
"haloo sauna vp tena"
"ulisema upo Dar"
"ndio"
"sasa kwanini ulinidanganya kua hutoenda dar, ivi kwanini ninyi wanaime ni waongo ivyo.... Ok upo Dar sehemu gani"
"mmmhh kitu kama ostabey hivi"
"heee Magomeni si kwa dada yobi au ndio umekubali kwenda kwake"
"sauna, mi napenda kuigiza sauna, hivyo ndio nipo kwa dada yako na sasa kuna filamu ambayo hivi... "
Alinikatisha maongezi yangu na kusema kua
"sitaki kujua kuna filamu au hakuna, sasa kwsho ni Jumamosi sio siku ya kwenda shule hivyo nitakuja asubuhi"
"heeee Uje? Lakini sawa si utakaa kwa dada yako"
"mimi siji kwa dada na staki ajue"
"afu kwanza anaumwa ile mbaya"
"staki kujua, si yeye mwenyewe kwanini asingenipigia simu kama ndugu yake"
"atakupigia na wakati ana hali mbaya"
"ok poa, kesho saa nne, nitakuja na fastjet, then ikifika saa 11 jioni nitarudi"
"mmmhh sawa"
Nilikubali kishingo upande mana huo muda wa kwenda kumchukua uwanja wa ndege mbona nitakua sina, ila nitafanyeje sasa mana Kiukweli ananijali haswa...
Usiku huo ulipita ambapo ndio tunaamkia siku ya Jumamosi, niliamka mida ya saa 2 hivi nikaingia bafuni kwa ajili ya kujiweka safi, baada ya kuoga nilimuita jeni,
"jeni, we jeni"
"abee bayby"
"we hilo jina la bayby limetoka wapi tena"
"kaka sheby? Samahani kama nimekuuzi ila inanitokea tu kukuitikia hivyo coz nakupenda sana sheby na ndio mana siku ile nikakuruhusu ulale na mimi, na nilishukuru sana ulitekeleza agizo"
"aahhh ok, vp chakula cha mgonjwa umeshakiandaa"
"yes kipo tayari"
"hebu nipatie mara moja niwahi mana nimechelewa sana"
Basi nilichukua chakula cha mgonjwa kisha nikakiweka vizuri katika gari, kisha nikawasha gari na jeni akawa anafungua geti tayari kwa kuondoka...
Lakini kabla sijatoka mara simu yangu iliita, kucheki aliopiga alikua ni dada wema
"haloo"
"Eeh halo boy mambo"
"poa shkamoo"
"ok, poa... Sasa sheby please please please my boy, please nimesahau nguo yangu huko kwenuu Please naomba uniletee nyumbani kwangu tafadhali sheby naona uvuvi kuja huko"
"ooohhh shit, mimi siji huko napeleka chakula hospitali kwa dada yobi"
"jamani sheby yani kupitia tu mara moja imekua nongwa"
"sorry my sister please naomba niwahishe chakula nakuomba"
"ok, nakukubalia... Lakini kumbuka kua utaileta mwenyewe hio nguo"
"ni nini kwani, ni gauni au sketi"
Nilijifanya sijui lakini kumbe najua vizuri sana,
"jamani sheby sio nguo hizo ni nguo kama ile ulioniletea siku ile"
"ayaaaaaaaa Aiseeee tabu gani izi jamani"
Nilikata simu kisha nikaendelea na safari yangu ya kwenda hospitali, Nilikua spidi sana hata alama za barabarani nilikua sizifati kabisa, Punde sii punde nilifika K/koo ambako ndipo hospitali hio ilipo, Niliingia wodini hapo ambapo ndipo alipolazwa dada yobi,
"shkamoo dokta"
"marahaba ujambo kijana"
"sijambo,... Aaahhh dokta hali ya dada leo ipo kiafya"
"aaahhhh Kiukweli tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kumpa nguvu dada yako, Kiukweli hali yake sio mbaya, na hata hii wiki sidhani kama atamaliza"
"heeeeee hatomaliza kwanini?"
Nilitoa macho kutokana na yale maneno ya dokta mana sikumuelewa alikua na maana gani kusema dada yobi hawezi maliza hata hii wiki
"Ahahahahahaha mbona wantolea macho hivyo kijana"
"maneno yako ayo dokta"
"Mimi nimemaanisha hatomaliza wiki ataruhusiwa kurudi nyumbani na kuendelea na kazi zake"
"Ah haaa kumbe ulimaanisha hivyo ee"
"yes"
"ok, basi akiamka uniite nipo hapo nje ili nimlishe msosi"
"aahh unampenda dada yako kweli kweli yani"
"yes, because she is my sister"
"i know but is too much for that"
"kwani dokta, kumpenda ndugu yako kuna kikomo"
"hakuna kikomo cha kumpenda ndugu"
"so why you Said is too much"
"acha ligi kijana, hebu tusije kumuamsha mgonjwa kapumzika"
Tulikua tukibiaha na dokta huku tukiwa na furaha, hivyo nikagundua kua upendo ninaompa dada yobi ulikua unazidi hadi watu wanashtukizia kua huenda sio ndugu hivyo yapaswa nipunguze ili wasishtukie sana,.... Basi nilikua zangu nimeketi hapo nje naplay game kwa phone yangu, huku nikisubiri dada yobi aamke ili niweze kumjulia hali na kadhalika,... Sasa nikiwa nipo hapo nje ya wodi aliolazwa dada yobi au kipenzi cha moyo wangu, simu yangu iliita na jina alikua ni sauna
"haloo"
"sheby mpenzi, nipo Airport nimeshafika"
"wahat, ivi ulikua unamaanisha kweli unakuja sauna"
"yes na nimeshafika now nipo naku wait"
"mmhh oookeee"
Nilikata simu na kucheki saa ilikua ni saa 5 hivi kasoro, Nikaona ngoja nikampokee yule mtoto wa watu kule airport,... Niliwasha gari na kuelekea huko mana licha ya kua mgeni lakini nakujua, kwasababu hata mimi nilipokuja nilikuja na fastjet,... Nusu saa mbele nikawa nimefika eneo husika ambapo ni airport, nilikua naangaza angaza macho huku na kule kana kwamba huenda nikamuona.. Ghafla nikaguswa kwa nyuma, kugeuka alikua ni sauna kumbe aliniona kabla yangu,.....
SAUNA NI MDOGO WAKE NA DADA YOBI, YULE ANAEUMWA... NI MDOGO WAKE KABISAA TOKA NTOKE NA SAUNA NDIO MTOTO WA MWISHO KWAO,... NA WA PILI NI ASNATI, NA WAKWANZA NI HUYU DADA YOBI... (ZINGATIA USICHANGANYE WATU HAWA)
"waaooo sheby umeanza kua mweupee"
Basi mtoto wa kike kwa furaha akanikumbatia tena kwa kuning'inia haswaa kwa furaha....
"mmhhh sauna umekua mzito, ivi nitakueza kweli na huu uzito"
"wewe usinipasue moyo wangu mie, wakati ndicho nilichokifata huku"
"mmhhh je kama sina"
"huna kiende wapi,... Yaani mfano mtu anataka kukichukua, niko tayari kukigharamia kwa kiasi chochote kile ilimradi uendelee kua nacho"
"mmmhhh we sauna muongo wewe"
"kweli sheby... Mimi toka nianze kiyajua mapenzi, sijawahi kufikiria mwanaume hata siku moja, na sijawai kuwaza kama ipo siku nitamfata mwanaume mkoani"
"kama maneno yako ni ya kweli basi nami pia hivyo hivyo"
"shebiiiii, nina hamu na wewe sijui nisemeje mie"
"ok sasa tunafanyeje kuusu sehemu ya kwenda, mana ulisema huendi kwa dada yako"
"ina maana sheby hujapangisha hata chumba"
"wala"
"kwahio, unalala na dada yangu nyumba moja"
"lakini ni ya rosheni mimi juu yeye floo ya chini"
"hata kama lakini si nyumba moja"
"ndio"
"staki tena uishi huko, na kama ni kukufundisha huo uigizaji si akufundishe tu, kwani lazima uishi kwake"
"lakini sauna mi namueshim sana dada batuli"
"najua, hata mimi namueshimu, ila kwa ulinzi wa penzi langu mimi na wewe, naomba uhame kwa dada batuli"
"lakini sauna, nitahamaje ghafla pasina taarifa"
Unajua mimi sitaki kuhama kwasababu dada yobi ni mpenzi wangu, hivyo nikimhama na yeye atajiskiaje, na hakuna anaejua kama dada yobi ni mpenzi wangu, hata huyu sauna hajui kitu, hivyo yeye anajua mimi nimekuja kufundishwa kuigiza kumbe, ni my sweetheart
"mbona ni kitu kidogo tu hicho sheby, unamwambia bwana dada mimi nimeona nipangiahe chimba changu lakini kuihiza kwako unaendelea"
"mmmhh ok nitajaribu"
Unajua nampenda sana sauna kwasababu anakunjuka sana kifedha, yaani hapa nikisema nataka laki mbili basi napewa laki tano....
KISOME HIKI KISEHEMU HAPA CHINI ILI BAADAE USIULIZE SANA MASWALI
HII FAMILIA CHIMBUKO LAKE NI LA KITAJIRI SANA TENA SANA, HIVYO USISHANGAE MTOTO WA KIKE KAMA HUYU AKINIPA MILIONI KUMI AU TANO, MANA NAKUMBUKA ALISEMA KUA AKAUNTI ZAO ZILIANZA KUWEKEWA PESA TOKA WAKIWA WADOGO, HIVYO MPAKA SASA WANA PESA ZA KUTOSHA KATIKA AKAUNTI ZAO HAWA WASICHANA WATATU.... DADA YOBI.... ASNATI.... NA HUYU SAUNA... WANA PESA ZA KUMWAGA NA HAPO HAWAJAOMBA KWA WAZAZI WAO, JE WAKIOMBA ITAKUAJE.... SASA TULIENI..
"ok kwa sasa naomba tuelekee kwenye hoteli yeyote nzuri"
Basi tulipanda kwenye gari hio ambayo ni gari ya dada yake, tuliondoka hapo airport na kuelekea Mbezi Beach, kwenye hoteli moja hivi kalii, na kama unavyojua Mbezi ni moja ya sehemu za mashavuni sana,... Tuliingia hotelini hapo na kuchukua chumba kimoja matata kina kila kitu ndani kasoro msosi, ila kuna sehemu ipo spesho kwa ajili ya watu aina zote kwa kupata msosi, yani kama hutaki kula peke yako chumbani basi kuna sehemu ya mjumuiko wa wote, na palikua panasifika sana kwa kuku na hata sisi ndio tulikua tunaelekea huko kujumuika kula na watu wengine, Sasa tulipokua tunashuka ngazi tena tukiwa tumeshikana kiuno,.. Ghafla nikamuona dada wema akiwa na mwanaume mmoja hivi il sijamuona vizuri, Sasa ilibaki tu kidogo tukutane uso kwa uso, hivyo nikajikuta nageuka fasta na kuangalia nilipotoka,
"we sheby una nini mbona unarudi juu tena"
Sauna aliniuliza huku akishangaa kwanini nilirudi ghafla, na uzuri ni kwamba wema hawajui wadogo zake na yobi zaidi ya mimi tu, hivyo nikawa nimempa mgongo ili asinijue kama nipo hapo,... Sasa mbaya zaidi yule dada wa pale mapokezi alikua hayupo, nadhani alielekea toilet, sasa nikaskia wanaulizana na huyo mwanaume aliokua nae
"oohh shit, huyu secretary yupo wapi tena"
Aliongea dada wema huku akionekana kusikitika sana... Lakini yule mwanaume alitoa wazo la kijinga kweli kweli, Eti alisema
"au hebu tuwaulize hawa watu ili tujue kama kuna huduma au hakuna"
"ooohh yes, wacha niwaulize mimi"
Mungu wangu eee sasa sijui itakuaje kama atataka kuniuliza mimi, mana akinijua kua mimi nipo hapo, tena niko na mwanamke, afu tena tunatoka juu huku tumeshika biuno,
"samahani kaka, naomba nikuulize"
Itaendelea..... after Tomorrow
KWA LOVE STORY ZAIDI YA HII BOFYA HAPA NCHINI UKAJIPIMIE,... ILA USISAHAU KULIKE PAGE HIO ILI USIPITWE NA VIPYA VIPYA →→→↓↓↓
https://www.facebook.com/pages/Moon-vision-Enter/571095712946246?ref=hl
USIKOSE HAPO KESHOKUTWA USIKU... MIDA KAMA HIII HAPA
0 Comment to "MWIGIZAJI BALAYA Sehemu Ya 15"
Post a Comment