Tuesday, February 13, 2018

SEKRETARI WA KIUME Sehemu Ya 11

SEKRETARI WA KIUME

Sehemu Ya 11

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/

Ilipoishia Jana...........

MWANAUME MASHINE

"ooohhh yeee, hhhooo my god... Yes baby... Hhhh... Uuuuuuuuuwiiiiiiii... Yesuuuu... Iiii... Aaaiiiiiiii"
Jafari alishtuka kuskia hizo sauti... Na alikua ni madam ndio kazitoa sauti hizo... Sasa Jafari yeye hajui kiwa madam aliskia hizo sauti jana alipopiga simu, ikajipokea wenyewe..
Saaa hata Jafari anashangaa sauti hizo Veep... Sasa Jafari kwa wenge akajikuta anasalimia, salamu ambayo madam haitaki
"heeeeeee Shikamoo madam"

"kamsalimie mama ako kama hio salamu inashibisha....... Yaani unaacha kazi yangu Unakwenda kufanya... Kufa... Kufa...kufanya....kufanya mapenzi.... Hivi unajua umeitia kampuni hasara kiasi gani kwa masaa yako mawili ulio ondoka hapa... Kwa ulivyo masikini huezi lipa milioni kumi wewe.... Sasa kuanzia leo, sitaki kuiona sura yako hapa... Mlango ulio ingilia naomba uutumie na kutoka..... Nafumba macho nikifumbua nisikuone hapa"

ENDELEA........



Madam nailah Aliongea maneno mengi bila kumeza mate, tena kwa hasira mno.... Afu hapo hapo akafumba macho, yaani ni kweli Jafari anatakiwa kutoka nje ya geti, na hapo kazi ndio basi tena... Jafari haamini kama leo ndio mwisho wa kazi yake... Na wakati huo madam kafumba macho huku machozi yakimtiririka kwa fujo.... Sasa Jafari ndio akakumbuka kuwa, pale madam alipopiga simu ilijipokea yenyewe, huku tv ikiendelea kutoa sauti za ile cd walioweka kule kwa aisha... Na ndio mana Jafari alipongia akakutana na sauti ya madam akiigilizia zile sauti.... Jafari akaona ngoja ajaribu kujitetea... Sasa ile anataka tu kuongea, mara madam kufumbua macho, tena yamekua mekundu kama kavuta bangi,.. Jafari akaona hapa hakuna cha kujitetea wala nini.... Jafari kashika mlango huku akiuliza
"najua nimefanya kosa Madam.... Lakini, mshahara wangu unanipa hapa au ndio sipati kabisa"
Jafari aliuliza swali hilo lililompa nailah hasira nyingi
"nasema tokaaaa"

Jafari alitoka chap chap kwenye kampuni ya watu,.. Kwanini ang'ang'anie na wakati anafukuzwa, hapo koridoni walijaa wafanyakazi wote wanamuona Jafari anafukuzwa kama mbwa kichaa,... Walianza kumcheka Jafari, lakini aisha alikuwa akilia sana kwa kitendo cha jafari kufukuzwa,.. Lakini hakutaka kumwacha atoke mwenyewe, alitoka nae kama kumsindikiza
"huyu aisha vipi, mbona anamfuata mhalifu"
Aliongea mfanyakazi mmoja huku mwingine akijibu
"huezi jua, labda wanajuana hao"
Aliongea mwingine huku wakicheka sana,...
"baby... Saaa mbona hujaomba msamaha baby wangu"
Aliongea aisha huku jafari akiwa kunyamaza tu,.. Mlinzi alifungua geti na kumruhusu jafari na aisha watoke nje, aisha alikuwa akilia mana kamzoea mpenzi wake hapo kazini, vituko vyake,.. Na hata pale kazini wapo waliohuzunika kwa kufukuzwa kwa jafari
"si nakuuliza jeff jamani"
"skia aisha... Madam alikuwa na hasira sana, hivyo asingeweza kunisikiliza kwa wakati ule"
"basi subiri nikajaribu kukuombea msamaha"
"hapana... Madam anakujaga nyumbani kwetu... Nitamuomba msamaha kule nyumbani"
"mmmhh sawa.... Lakini fanya juu chini baby urudi"
"Usijali"
Basi aisha alirudi kazini na jafari akasepa zake

Ofisini Madam alikuwa kajiinamia kwenye meza analia sana, mana mtu kamuamini anampa mpaka kazi za siri azifanye lakini anadiliki kuacha kazi anakwenda kufanya mapenzi, yaani madam kila akiwaza jambo hilo hapati picha kabisa,.. Hapo ofisini hatulii, hata kazi haziendi kabisa kwa upande wake...

Huku kwa wafanyakazi wanajiskia raha sana, mana kampuni nzima mfanyakazi boya boya alikuwa ni jafari, elimu hana... Hata cheti cha kidato cha nne tu hana... Wale waliokuwa wakihuzunika sio kwa kua jafari kufukuzwa, bali walikuwa wanasikitika kwa maana ile hali ya kuitwa itwa na madam itajirudia tena, mana toka jafari aanze kazi hapo, hakuna mfanyakazi alio itwa itwa mara kwa mara,.. Kwani kazi zote alikuwa akizifanya jafari,... Huezi amini madam kweli alimuamini sana jafari mpaka kazi za siri anampa afanye yeye, na kamfundisha mpaka kajua,..

"haya saa hizi kuna nini... Au boss wako kakutuma"
Aliongea Mwajabu au mama yake jafari, baada ya kumuona jafari anarudi kazini saa tatu asubuhi,
"kimenuka huko"
Jafari alimwambia mama yake, lakini mama nae alikuwa mwepesi,.... Kiliskika kibao tu
"taaaaaaaassssssss"
Jqfari amebaki kushika shavu tu,.. Hakujua kama hio ishu ingekuwa kubwa kiasi hicho,
"we mshenzi sana.. Nilikwambia utarudi mtaani acha mchezo na kazi husikii... Haya kavute bangi sasa.. Pumbavu wewe"
"mama, lakini hakujabadilika kitu... Mimi hata zege nitakwenda kukoroga wala siogopi... Mama umezaa dume we subiri.. Kwanza kazi yenyewe nguuumu"
Aliongea jafari huku mama akimguata jafari na kumwambia
"Unasemaje wewe... Kazi ngumu kwasababu umefukuzwa... Usinieleze upumbavu wako mimi... Najikakamua kumheshimu mtoto mdogo kama yule ili mwanangu upate kazi,.. Umekosa kusoma mpaka kazi nayo umeikosa... Mshenzi wewe"
Mama kachafukwa mno, lakini pamoja na kufanya makosa yote hayo mama aliendelea kumpa kazi... Mana ni mtoto wake, hana jinsi na hawezi kumtupa....
"nenda kanichukulie nyanya na ndizi mbivu... "
Mama alimtuma mtoto wake sokoni, na jafari anajua kuwa akiwa nyumbani lazima amsaidie mama yake kwenda sokoni, na hilo kwake halina tabu
"sawa... Ngoja nichukue gari yangu"
Aliongea jafari huku akitoa baisikeli yake
"umeshazoea kuendesha magari ya kifahari,.. Utaweza hio baisikeli"
"aahhhh mamaaaa.... Miezi sita tu kwenye magari, inifanye nisahau kuendesha baiskeli"
"angalia usije ukagongwa na magati baba.... Afu uwahi kurudi mana kibanda hakina nyanya hiki"
Aliongea mama wakati huo hasira zimeisha mana huezi muekea mwanao kinyongo muda wote, kama kakosea keshakosea tu.... Mtoto akiunyea mkono, safisha kisha endelea na kazi...

Jafari alikwenda sokoni na alirudi, lakini siku hio hakutaka ipotee bure mana bado ni mapema
"sasa mama... Nataka nikatafute kile chumba..."
Aliongea jafari huku mama akimshangaa sana
"sasa mwanangu, kwa sasa kazi huna... Ukitafuta hicho chumba utakilipa na nini baba"
"mama... Wacha nitafute chakwangu tu kwanza..."
Lakini sasa mama akagundua kuwa akikaa mbali na mtoto wake, lazima aanze kujichanganya na makundi ya kihuni, kwasababu atakuwa hana kazi sasa lazima akajichanganye na makundi mabaya ya kihuni
"sitaki,.. Utalala hapa hapa... Utakula hapa hapa, na tutaishi wote hakuna kwenda.... Kama hio hela huna kazi nayo nipe niongeze mtaji"
"mamaaaa.... Lakini mimi nimeshakua mama"
"kukua huko vepe... Hata kama ungeota ndevu kama osama... Nitaishi na wewe mpaka ufe... Kw sasa huna kazi siwezi kukuachia ukakae peke yako huko"
Aliongea mama huku akiendelea kupanga nyanya kwenye kibanda chake cha mboga mboga matunda ya kila aina... Yaani kama vile yupo sokoni...
"lakini mama"
"nimesema sitaki"
Mama alikataa katu katu,... Na jafari hakutaka kulazimisha alichukua baiskeli yake, kaenda zake kijiweni kwa kaka yake wa mtaani...
"aaahhhh kaka kaka, shkamoo bro"
"marahaba jeff mambo vipi"
"safi brooo... Naona una kazi nyingi hapa, hebu ngoja nikusaidie"
Aliongea jafari mana hapo kuna kagereji ka baiskeli.. Hivyo leo fundi kapata kazi nyingi afu yupo peke yake hivyo jafari akaanza kumsaidia,
"afu mbona saa hizi upo huku, au una off"
Aliongea fundi mana jafari anapitaga hapa hapa kwenda kwao akiwa anaendesha gari ya madam, na madam pia akiwa ndani.. Hivyo fundi anajua kuwa dogo lake ana kazi nzuri tu ya kumuendesha boss
"aahhh broo we acha tu... Kazi za wanawake hazidumu kabisa yani"
"kwanini useme hivyo"
"mwanamke ukimfanyia kosa, hata kama sio kweli lakini anashindwa kukuamini"
"kwani kuna kosa gani dogo langu"
"aahhhh makosa ya kawaida tu kuchelewa kazini, sasa yeye kaona nimefanya makusudi"
Jafari alikuwa akiongea huku anachapa kazi na wakati huo inakwenda mida ya saa tisa hivi alasiri... Na jafari hua haongei ukweli mana ni kwei kafanya kosa, kaacha kazi kaenda kwa mwanamke... Kufika kule wakaweka mikanda ya ngono,.. Kapigiwa simu ikajipokea wenyewe wakati simu ipo mfukoni katika ile hali ya kuminyana minyana ikajipokea, madam akasikia sauti za mapenzi zilizokuwa zikitoka kwenye video, na sio kuwa ni wao, japo nao walikuwa wakijiandaa kwa kazi hio lakini ilikuwa bado.... Sasa hilo ndio kosa la jafari na hawezi kulisema kwa watu mana ni kosa la kweli, ila madam yeye hajui kama zile sauti zilikuwa ni za video....

Saa kumi na mbili na nusu jioni madam anapita pale pale jafari alipo, mana ndio njia ya kuendea kwa akina jafari kula kachumbari, hivyo ni lazima apite hapo kwa waziba pancha za baiskeli na magari,.. Sasa madam kupiga jicho kamuona jafari, wakati huo jafari yeye yupo bize na tairi ya gari... Mana kuna tairi limeletwa lizibwe pancha, sasa jafari alikuwa bize kweli kukagua pancha ilipo hivyo hakumuona madam, lakini madam kamuona jafari anapigika na kazi,... Tena alikuwa na furaha sana jafari wala hakuwa mtu wa hasira labda kuwaza kuwa kufukuzwa kazi, yaani yupo simpo sana.... Madam alipita zake wala hakutaka kujulikana kuwa ni yeye kapita hapo... Na hata kaka yake jafari hajamuona tajiri wa jafari kuwa kapita hapo... Lakini madam anashangaa mtu kamfukuza kazi lakini bado hajutiii tu...

Huku nyumbani madam ndio kafika, mama kama kawaida yake kumpokea kwa heshima zote,.. Lakini mama leo hakutaka kuongea jambo lolote kuhusu mtoto wake, mana alishamuombea msamaha, hivyo hakupenda kuomba tena mana itakuwa kama anajishusha sana na yeye ni mtu mzima, kumbembeleza mtoto mdogo kama huyo kila mara sio vizuri, hivyo mama akapiga kimyaa...
"mama, leo upo kimya mama"
Aliongea nailah baada ya kuona mama jafari anaandaa kachumbari
"eeehh ahh wala tu sema sijiskii vizuri"
Aliongea mama huyo, lakini madam akajua mama haongei kwasababu kamgukuza mtoto wake...
"lakini mama.... Mtoto wako umemlea vizuri sana... Nimependa malezi yako... Lakini kuna kitu Umesahau kumfundisha mwanao"
Aliongea nailah huku mama akishangaa maneno ya nailah
"kwanini? Na kipi sijamfundiaha"
"mwanao hajui kuomba msamaha hata kidogo... Nimemgombeza kama mdogo wangu, lakini hata kusema dada Nisamehe, hajasema.... Nami nilikuwa nasubiria msamaha wake nimsamehe, lakini kagoma"
Sasa mama hapo ndio akapanda nguvu ya kuongea
"ina maana hajakili makosa yake"
"hajajigusa hata kidogo mama"
"huyu mtoto ana nini lakini"
Aliongea mama, na ni kweli pale kwenye kufokewa jafari hakuomba msamaha zaidi ya kuulizia mshahara wake tu basi....
"mi sijui na ni mzuri kwenye kazi"
"mama... Basi naomba umsamehe tu, asije kujiunga na makundi ya kihuni"
Aliongea mama yake jafari baada ya kugundua kuwa kumbe jafari angeomba msamaha, angesamehewa.. Hivyo mama akamuombea msamaha badala yake
"nakuheshim sana mama.... Basi akija mwambie kesho arudi kazini"
Aliongea madam boss, kuwa jafari kesho akija arudi kazini...
"Ahsante mwanangu... Yaani kesho namtimua asubuhi asubuhi"
"sawa mama.... Vipi kachumbari tayari"
"eeehh mama kipo tayari"

Sasa huku kwa waziba pancha,... Kuna gari aina ya hilax moja mayai dabo kibin, iliingia pale mida ya jioni sana,... Fundi alijua hio ni kazi...
"dogo langu, tengeneza hela hapo nipo bize huku"
Fundi alimtuma jafari aongee na huyo mwenye gari alio ingia hapo, agu mafundi hua wanajua kazi kweli, ni kama kinyozi.... Ukiingia saluni jicho lake kichwani.. Anajua umekuja kunyoa.. Sasa fundi pancha akiona gari tu, macho yake yanakimbilia kwenye matairi mpaka akaona kuna tairi imebonyea kidogo..... Sasa jafari alilisogelea gari hilo kisha akamsubiri tajiri ashuke.... Alishuka bidada mmoja hivi, mwenye umbo kama la madam boss na hata kiumri huenda wakalingana... Tofauti yao ni rangi ti, madam nailah yeye ni mweupe, ila huyu ni maji ya kunde hivi, nguo alizovaa ni balaaa...
"za saa izi kaka"
Alisalimia dada huyo kisha jafari akaitikia
"salama tu dada angu... Karibu"
"Ahsante.... Samahani kaka, naomba unijazie upepo"
Aliongea dada huyo huku jafari chap chap akaenda kuwasha komplesa ya upepo na kuanza kujaza lile tairi,... Lakini yule dada alikuwa akimwangalia sana jafari kama vile anamjua hivi...
"Samahani we kaka,... Kama vile sio mgeni machoni mwangu"
Aliongea yule dada huku jafari akiwa bize na valvu ya upepo,..
"sina uhakika saana... Ila huenda"
"wewe, kama nilikuona ukiwa na nailah"
Sasa jafari kuskia hivyo akajua kweli huenda anamjua, mana kama kamjua boss wake, basi ni kweli anamjua...
"basi unanifahamu lakini mimi sijawahi kukuona"
"ni siku moja ulikuwa unampeleka nailah kwao... Wewe si dereva wake"
"ndio ni mimi"
"sasa kwanini uko hapa"
"aahhh si unajua kazi zenu bwana... Hua mpaka mtuamini itachukua muda sana"
"ahahahahahahaha amna bwana sio wote... Kwahio kwa sasa huna kazi"
Aliongea dada huyo huku jafari akimalizia kufunga valvu kepu katika rimu ya gari hio...
"ndio.. Nipo hapa napiga piga na braza wangu hapa"
"ooohh ok... Sasa vipi, unaweza kuwa dereva wangu, mana hata mimi natafuta dereva ujue"
Jafari kuskia hivyo, akaona bahati gani hii, kwacha kazi leo afu anapata kazi leo leo.. Lakini jafari akaanza kujifanya kujivuta vuta ili na huyu asije akamlipa laki moja kama madam nailah...
"aahhh nyie mishahara yenu sio mizuri... Kama yule mi alikuwa ananilipa laki mbili tu"
Jafari alidanganya kuwa madam nailah alikuwa akimlipa laki mbili wakati ni moja tu ndio aliokuwa akilipwa...
"Usijali mimi nitakulipa laki tatu"
Jafari kuskia laki tatu, wooooohhh alitamani kumkumbatia yule dada lakini akasita kwakua ndio wamekutana saa hio.. Lakini huyu dada aliona kabisa jafari kanyanyua mikono ya kumkumbatia afu kasita,.. Dada alijua jafari muoga... Akamkumbatia yeye... Jafari haamini kama kakumbatiwa na boss wake mpya, mana madam nailah mpaka umkumbatie hivi ni shughuli pevu..

Sasa wakati wamekumbatiana, mara madam nae ndio anarudi kutoka kwa akina kafari,... Saa ngapi hajaona kumbatio la jafari na huyo dada... Afu sasa kumbe madam nae anamjua huyo dada
"Shantel.... Mmiliki wa madanguro hapa mjini.... Hapana.... Haiwezekani"
Madam nailah alilitaja jina la dada huyo huku akisema haiwezekani, kana kwamba huyo dada sio salama kwa Jafari, mana huyo dada anamiliki madanguro yaliojaa wasichana, halafu mbaya zaidi hua anawatumia wavulana wenye nguvu kurekodi video za ngono na kwenda kuziuza nje ya nchi,... Na vijana wengi huwachukua kwa niia ya kuwapa kazi za udereva.... Sasa madam nailah kaliona hilo... Kashika simu yake na kumpigia mama yake JAFARI...
"hallo mama"
"eeehh rehema mwanangu"
"mama... Hebu mpigie simu mwanao sasa hivi mwambie arudi nyumbani sasa hivi"
Aliongea madam nailah wakati huo  Shantel anaingia ndani ya gari kutoa malipo ya kazi aliojaziwa pepo... Na wakati huo nailah anaona live bila chenga mana tayari kagiza kameanza kutanda..
"kwani kuna nini mwanangu"
"mpigie sasa hivi utampoteza mwanao yupo kwenye hatari"
Aliongea nailah tena alikuwa akilia sana, yaani roho inamuuma na anajuta kumfukuza kazi... Mana kaja kuingia pabaya...
"sawa hebu kata simu"
Sasa mama JAFARI nae presha kwa kuskia mtoto wake yupo kwenye hatari....
"boy, njoo uchukue malipo yako"
Shantel alimuita jafari kule kwenye gari,... Madam nailah haamini kama jafari anaingia kwenye gari, sasa madam anajua kuwa jafari ndio anaingia wanaondoka.... Nailah alishuka kwenye gari ili kwenda kumzuia jafari asiondoke... Lakini sasa ile anavuka tu barabara,.. Ghafla kuna gari iliachiwa huko na spidi kali,.na madam alikuwa anavuka barabara, Maskini madam alibaki tu kuduaa hapo barabarani, kukimbia kashindwa, kabaki kusimama katikati ya barabara.... Iliskika tu sauti ya kilio
"uuuuuuwiiiiiiiiiii"

GHARAMA YANGU NI SHARE 200 TU,
ZITAKAPOFIKA TU, NAENDELEZA...

www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/

STORI ZANGU ZOTE HIZI HAPA....

(1).KIJAKAZI WA KIUME

(2).MLINZI WA GETI

(3).DEREVA TOYO

(4).MTOTO WA HAYATI

(5).ONE DAY YES

(6).SECONDARY SCHOOL

(7).FUNDI CHEREHANI

(8).MWIGIZAJI BALAYA

(9).THE DOM

(10).THE ISLAMIC WIFE

(11).MKE JEURI

(12).YOUNG PASTOR

KUZISOMA ZOTE, BONYEZA HAPA
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/

AU.... NICHEKI KUPITIA NAMBA +255714419487 WhatsApp

Utazipata Zote Mpaka Mwisho Kwa Simu No: +255714419487 WhatsApp, Au, Like Page Yetu Ya Facebook Kwa Kubonyeza Hapa Chini ili Usipitwe
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/

tAfBoy {.Tanzania's Frugal Boy..}

Share this

0 Comment to "SEKRETARI WA KIUME Sehemu Ya 11"

Post a Comment