{The Prostitute Actor}
Sehemu Ya 24
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Ilipoishia Jana →↓↓↓↓â†
"ivi anty sasa nifanyeje nimpate uyu mtoto mana ananisumbua afu dada yake ndio kikwazo sana"
Ilikua ni sauti ya wema akiwa anaonge na rafiki yake Anty Ezekieli,
"kama vp nenda kwa babu"
"mmmhhh hapana mi sipendi mapenzi ya kwa mababu mana dawa zikiisha hua yana zalilisha sana"
"ah ah mimi simaanishi umuendee huyo kijana... Ila namaanisha uende kwa ajili ya huyo kikwazo wake"
"you mean dada yake"
"yes"
"mmmmmhhhhhh"
"hio ndio nja, na bila hivyo hutompata"
Wema alimaliza kukumbuka moja kati ya ushauri alioupewa mchana, Ikiwa ni mida ya saa 8 usiku akiwa kashika simu yake aliotaka kumpigia mtu fulani.... Alijikuta akikumbuka tena neno la mwisho aliloshauriwa na anty kua
"na ukitaka kufanya hivyo hakikisha unampigia babu mida ya saa 8 na nusu usiku (2:30), na ikipita na nusu basi haitowezekena tena hadi siku nyingine muda kama huo"
Wema alimaliza kukumbuka kisha akaangalia saa yake iliokua ukutani na kugundua kua muda huo, ulikua ni muda wa saa 2:29 (saa nane na dakika 29) yaani bado dakika moja tu ili aweze kupiga simu kwa babu....
Wema Alikua makini sana na ile saa kwa kuisubiri dakika hio itime.... Na ni kweli ilivyotimia tu saa nane na nusu usiku, alibofya simu yake kisha akaiweka sikioni, na simu ilikua ikiita usiku huo... Sekunde chache mbele simu inapokelewa na dada wema anaanza kuongea au kunuia maneno kwa kutumia simu....
ENDELEA.............
Sasa maisha yanaendelea kua ya kidigitali zaidi kuliko zamani, mana kama unaweza kumuua au kumfanya mtu chochote kwa kutumia simu, hii ni moja ya maendeleo kwa nchi yetu, kumbe ukipiga simu kwa mganga anaweza kurekebisha mambo kwa mhusika,
Wema akiwa chumbani kwake alikua akiisubiri dakika ya mwisho kwa ajili ya kupiga simu kwa mganga wa jadi ili kuweza kumfanyia chochote batuli, Akikumbuka ushauri alioupewa na rafiki yake anty Ezekieli, kua ifikapo saa 8 na nusu usiku aweze kupiga simu ili kumfanyia chochote yobnesh.. Ghafla ilitimu mida ya saa 8 na nusu usiku na wema hakuchelewa kuinyanyua simu yake na kuanza kupiga kama alivyopewa ushauri na rafiki yake....
Punde sii punde simu ilikua inaita na hatmae kupokelewa na maongezi yalianza kuzungumwa
"mmmhhh shost mi nashindwa kufanya hivyo"
Ilikua ni sauti ya wema ikimpigia rafiki yake huyo ambaye ndio alimpa ushauri
"basi we huna shida"
"mmmhhh kweli anty siwezi, yaani nikifikiria tulioyafanya miaka yote, nashindwa, yule ni rafiki yangu aiseee I can't to do that"
"mmmhhh ok usiku mwema... Ila umeniuzi sana mi najua ushamaliza mambo kumbe umeshindwa"
"kweli nimeshindwa shost... But thenx kwa good Idea mana siwezi kumuumiza mtu kisa mapenzi"
"ok poa basi usiku mwema shost"
"ok nawe pia my"
Walimaliza kuongea kisha wema aliachana na jambo hilo na kuendelea kulala mana ilikua yapata saa nane na dakika 45 usiku, yaa dada wa sheby aliponea chupu chupu katika mikono ya wema, na yote hayo kisa ni mapenzi,
Baada ya siku hio kupita tukiwa katika mjengo wa yobnesh au batuli wakiwa ndio wapo mezani wakipata supu yeye na dada yake,
"sheby, jana umefanya poa sana... I love you my dear"
Alikua ni yobi akimsifu mdogo wake au mpenzi wake kwa kazi alioifanya usiku uliopita,
"yaani hapa nilipo magoti yananiumaa, kiuno ndo usiseme... Sheby mpenzi wangu... Sijui nikupe nini, mana unanipa kile roho inapenda kwakweli... Na wala sitaki kukubania kitu chochote sheby.. I love you so much my boy"
Kijana sheby alikua akipokea sifa zake kutokana na shughuli alioifanya usiku wa leo, yaani amemfurahisha sana dada yake huyo au mpenzi wake... Supu ilikua ikiendelea kuliwa kwa madaha huku mikonyezo ya macho yao yakiwa yanajibizana haswa,
Walimalia kupata supu, kisha walitoka zao wote na gari hio ya dada yake, mana ile mpya hatakiwi kuigusa kabisa yani, kisa tu imenunuliwa na wema,... Walitoka na kuelekea saloon mida ya saa 6 hivi mchana, walienda kutembelea baadhi ya biashara zao,.... Sheby aliachwa katika duka la nguo ili kuweza kukamilisha mahesabu ya kilichopatikana ndani ya wiki,.. Na dada yake nae alifuatilia jambo lingine la kibiashara.... Wakati kijana sheby akiendelea kupiga mahesabu ya duka hilo, mara simu yake iliita, namba iliopiga ilikua ni ngeni lakini alikua akiikumbuka kidogo
"haloo"
Alianza kijana sheby, huku akiwa makini kumsikia mpigaji
"haloo mambo sheby"
Ilisikika sauti ya kike, ilio nyororo sana
"poa nani mwenzangu"
Sheby aliuliza mana hamjui lakini mpigaji anamjua haswaa
"jamani sheby samahani, ni mimi Jamila rafiki yake na pau"
"aahh we si nilikuambia ufute namba au sio wewe"
"mmhhh sorry, nilikua nina maongezi na wewe Please"
"maongezi gani,.. Na pia unaweza ongea tu mana nipo bize kidogo"
"tafadhali sana naomba tukutane pale TAI RESTAURANT tupate hata lanchi pamoja"
"ok, nikipata muda nitakushtua"
"ok, ngoja nikutumie vocha ya kunishtulia pamoja na nauli kabisa"
Kiukweli kijana alikua ana bahati ya kuzipata fedha kwa kupitia wanawake.. Haijapita dakika mbili, mara simu yake iliingia meseji ya m-pesa.. Kuangalia vizuri alikua ametumiwa kiasi cha shilingi laki moja kisha hapo hapo simu yake ikaita tena,
"haloo"
"Haloo sheby,.. Elfu 50 tumia vocha na elfu 50 nyingine itumie kwa nauli ya kijia huku"
"ok poa"
Sheby alishangaaa kuona upepo wa pesa kama huo ukimuangukia,
"vp sheby kuna tatizo"
Aliuliza John ambae ndio muizaji wa dox hilo,
"hakina kaka, ila Nashangaa mtoto simjui lakini imeingia laki"
"aaahh, acha utani"
"sure kweli, hata sms hii hapa kaka"
"aaaaahhh Ebana zali iloo"
"amna kitu chochote"
Basi ni utani kati ya john na sheby kwa kuambiana mazari ya pesa,... Kwelo sheby hakutaka kulipuuzia hilo, ilipofika mida ya saa nane mchana alipigiwa simu na kuambiwa kua dada huyo keshafika tai restaurant, na sheby pasina kuchelewa alichukua tax kisha akawahi TAI RESTAURANT
Alipofika tai aliingia mpaka ndani ambako palikua na watu wengi sana waliokuepo eneo hilo, sheby alinyanyua simu na kutaka kupiga, lakini ghafla aliguswa kwa nyuma, huku aliomgusa akisema
"nipo hapa baby"
Sauti hio haikumshtua sana mana alikua akiifahamu kupitia simu,.. Alipogeuka alikutana na mtoto mzuri sana aitwae jamila, na jamila huyo ni rafiki sana na paula,
"ooohh mambo"
"safi tu, karibu meza yetu ile pale"
Kijana sheby hakutaka kujivunga,.. Jamila alikua na rafiki yake mmoja hivi nae alikua sii haba katika swala la uzuri, mana alikua kama shombe shombe hivi,
"mambo ahem"
Sheby Alisalimiwa na yule rafiki wa jamila, mpaka sheby akatabasam tu huku akiitikia
"poa nambie mamy"
"safi tu"
Mara jamila alidakia na kumuambia rafiki yake kua
"mmmhhh na wewe umewahi kumtukuza kabla bado"
Alimuambia hivyo kumaanisha kwamba yule rafiki wa jamila aliwahi sana kuniita mimi shem, na wakati bado mambo hayajawiva sawasawa, Japo jamilia alikua kajaaliwa kua na umbo alilotakiwa kua nalo mwanamke kama huyu, mana jamila sura alikua nayo, umbo ndio usiseme, jamila alikua na macho ya kumbutia kila mwanaume ambaye alikua ni rijali haswa,
Sheby aliandaliwa kinywaji murua na mschana huyo, huku akimuambia rafiki yake kua ampishe dakika mbili ili aweze kuzungumza na kijana huyo
"jesca"
"abeee shost"
"give me a one minute please my"
"ok, don't worry about that"
Basi jesca aliondoka kisha sheby akawa anaona aibu pale alipo, japo mdada huyo haikua mara yake ya kwanza kumuona,
"sheby... "
"sema"
"mbona kama una wasiwasi hivyo, au unamhofia wifi yangu nini"
Jamila Alimuambia sheby hivyo kama kianzio cha maongezi yake,
"wala tu, nipo fresh mbona"
"aahh nikajua labda unamuwaza wifi"
"mmmhh bado sijajaaliwa kua nae"
Sheby nae alizidi kujifungulia mlango ili mtoto wa watu aingie pasina kubisha hodi, unajua sheby amechanganywa na ile laki ya vocha na nauli, sasa moyo wake hapo ulipo anatamani atongozwe na huyo mtoto wa kike, ili vile vilaki laki visimpitie mbali,
"mmhhh we muongo, Kwanini usimpate"
"aahh sema mi mwenyewe nipo bize sana na mambo yangu"
Sheby alijifanya yuko bize lakini haikua kweli ila alikua anajifanya kuweka ugumu ili mtoto wa kike asigundue kua, anatamani kua nae...
Sasa mtoto wa kike keshaanza kua domo zege, alikua akimuangalia tu kijana wa watu huku akiangalia meza mara amuangalie mara ajishike shike vidole,.. Aahh si unajua wasichana wa kibongo mapaka akuambie hisia zake hua ni nadra sanaaaa, na pia haikua maadili ya kitanzania kumwambia mwanaume kabla yake, hivyo jamila alikua akitumia vitendo haswa macho yake, yaliokua yakimuangalia sheby kisha anayatoa,... Sasa dakika chache mbele mara jamila akadondosha simu yake chini, afu pale alipokaa jamila amejibana sana kana kwamba hawezi kuinama na kuiokota kutokana na meza na viti vilivyo banana, hivyo sheby kwa ushapu aliinama na kuichukua, lakini akiwa anaamka kutoka chini ya meza, alishangaaa kuliona jina lake huku chini ya meza... Yaani pale chini ya meza kulikua na ujumbe kwenye karatasi uliokua ukisema
"Sheby,... Ni mimi jamila naogopa kukutaamkia kua nakupenda... I love you sheby,... Please naomba uupokee moyo wangu"
Ujumbe ukawa umefika, lakini cha kushangaza sheby aliinua kichwa kutoka chini ya meza akiwa amekasirika,... Jamila alikua kavuta tabasamu lake zuri sana lakini ghafla likapotea baada ya kuiona sura ya sheby ikiwa imebadirika,.. Sheby alimpa simu yake kisha akatulia,.. Jamila alianza kuingiza uoga kana kwamba labda kuna kitu kakosea kuufikisha ujumbe,... Jamila bila kuchelewa aliandika meseje kwenda kwa Jesca, mana Jesca yupo hapo hapo TAI RESTAURANT,
"Jesca jamani, njoo naona sheby kakasirika ghafla"
Jesca nae alikua na kamchepuko chake kwa pembeni hivyo hakua na muda wa kuja ila waliongea kwa sms tu
"kwani umemfanyeje tena na wewe"
"mi sijui, nimefanya kama ilivyotakiwa lakini kanyanyuka akiwa na hasira"
"mmmhhhh na wewe jamila, ina maana na uzuri wako wote unashindwa kukashawishi hako kajitu"
"Eeeehhh Jesca tafadhali sana usiniitie mpenzi wangu kajitu"
Walianza kubishana mambo mengine tofauti na yale walitaka kuambiana...
"kwani kaku kubalia"
"hata kama lakini sio kajitu bwana"
"Ok sorry kwa hilo... But ebu tumia umwanamke wako akubali"
"ok poa"
Waliacha kuchati, Jesca na Jamila.. Lakini ghafla sheby alinyanyuka na kuelekea toilet, Jamila hakutaka kuchelewa, akaona hio nayo huenda ni moja kati ya nafasi yake, hivyo naye alifata nyuma na kusahau kua anakoelekea ni upande wa choo cha kiume... .... Je nini kitatokea huko
Itaendelea..... after Tomorrow
KWA LOVE STORY ZAIDI YA HII BOFYA HAPA NCHINI UKAJIPIMIE,... ILA USISAHAU KULIKE PAGE HIO ILI USIPITWE NA VIPYA VIPYA →→→↓↓↓
https://www.facebook.com/pages/Moon-vision-Enter/571095712946246?ref=hl
USIKOSE HAPO KESHOKUTWA USIKU... MIDA KAMA HIII HAPA
0 Comment to "MWIGIZAJI BALAYA Sehemu Ya 24"
Post a Comment