Wednesday, November 29, 2017

MWIGIZAJI BALAYA Sehemu Ya 1

MWIGIZAJI BALAYA

{The Prostitute Actor}

Sehemu Ya 1

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

Sasa siku hio ilikua ni siku ya kikao cha usiku, baina ya watu wote.. Yaani familia nzima na alioitisha mkutano huo ni dada batuli kana kwamba ndio anataka kuliongelea lile swala la mimi kwenda Dar es Salaam...
Na mimi nilikuepo kwa pembeni nimewategea tu skio langu,...
"ndugu wazazi wangu wapendwa... Leo nimewaita hapa nina ombi moja kwenu japo sio la muhimu sana jwenu....  Aahhh kama mnavyojua kazi zangu mimi ni uigizaji, na katika tasnia yetu hua hatuweki mtu ilimladi mtu bali tunaangalia kipaji cha mtu ili aweze kukava ile nafasi husika, na nimeona kuna nafasi sheby anaiweza...."

Kila mmoja alianza kutoa macho huku mzee mwenyewe akiuliza, kua
"Uu..u..uu...unasemaje we mtoto"
"baba na ndugu zangu wote... Nataka niondoke na sheby, tukaishi Dar es Salaam ili akijue kipaji chake... "

Mara mzee akaamka kwa hasira huku akisema,...
"wewe yobi wewe... Ishia hapo hapo na huko kuigiza kwako, inamaana Tanzania yooote hii umemuona sheby tu kua anaweza kukava huo ujinga wenu,... Sasa sikia ukitaka nikuachie laana ondoka na huyo kijana.. Pumbavu wewe... Nyiiiiaaaau we"
Afu mzee akaondoka zake kuelekea chumbani....  Mara na Asnati na akasema
"yaani dada yobi katka siku ulizo ongea pumba ni leo, yaani kama na mimi nina uwezo wa kukupa laana ningekupa wewe"
Hajakaa vizuri mara na sauna nae... Kaamka huku akisema
"hata mimi nimekuchukia ghafla tu dada angu, na ukitaka tuelewane muache sheby wetu"

Akiendelea kushangaa shangaa, mara na mama nae kaamka na kusema
"Huo upumbavu wako huo, upeleke huko huko dar kwenu, lakini sio sheby, wewe ni mtoto wangu lakini kwa swala hili nitakuchukia milele"
Mama aliondoka zake na kumfata mumewe huko chumbani kwao... Sasa tukabaki wenyewe, huku dada yobi akibubujikwa na machozi,... Alikua akijiuliza mengi sana lakini hakupata jibu..

"iv sheby, umeipa nini familia yangu... Nijibu umewapa nini hawa watu"
"mi sijui dada yobi"
"sheby, niambie ukweli, una mahusiano ya kimapenzi na familia yangu.. Hii sio bure kama sio mahusiano basi kuna kitu umewapa....... Sheby,  umetembea na familia yangu... Si kweli ee??"
"sasa kama nimefanya mapenzi na familia... Kwaio una maanisha hadi baba yako si ndio eeee"
"Ehh basi nisamee mpenzi wangu, huko umefika mbali sana... Basi nisamee kwa maswali yangu... Ila hebu nishauri tufanyeje sasa, mana licha ya wao kukataa lakini sintokuacha hata mara moja"
"we yobnesh? Umesahau baba ako kasemaje"
"hata kama lakini sikuachi sheby wangu"
"kumbuka laana ni mbaya dada yobi"
"sawa nipo tayari kuipata... Lakini wacha niwe na maisha yangu yote.... Hebu nipe njia tufanyeje ili tuondoke... "
Nilipata wazo moja nikaona ngoja nimshauri kama atakubali
"ok... Nina wazo ila utakubaliana naloooo"
"nipo tayari hata kama linagharimu pesa kiasi gani"
"wala haliitaji hata senti tano"
"ok skia sasa.........

SASA TUENDELEE NA MWENDELEZO WAKE....  KWANI HUO ULIKUA NI MWISHO WA STORY ILIOPITA.. NIMEIWEKA NDEFU ILI ALIEANZA HAPO AIELEWE VYAMA.......  SASA TWENDE KAZI

ENDELEA...........




nilitamani hata mimi niende dar es Salaam mana sijawahi kufika kabla...  Hivyo hata wazo amblo ningelimpa lilikua zuri ila sijui kama angekubaliana nalo...
Wakati huo dada yobi alikua akilia sana kwa kuishangaa familia yake ikimkana kisa mimi tu, na kujiuliza maswali mengi ambayo hata majibu yake hana,...  Ila kwa utamu wa dada yobi ilinifanya nami nikubali kwenda nae, tena nitaishi nae nyumba moja.. Yaani nitakua najisevia tu mwenyewe......

Nilipata wazo moja nikaona ngoja nimshauri kama atakubali
"ok... Nina wazo ila utakubaliana naloooo"
"nipo tayari hata kama linagharimu pesa kiasi gani"
"wala haliitaji hata senti tano"
"ok skia sasa.... Itabidi we uwaombe msamaha woote, afu uwaambia sawa umekubali kuniacha"
"What?.... Wazo gani sasa ilo"
"ndio... Na usiponifata mimi utalaanika kisa mapenzi".
"ok sawa... Sasa baada ya kuwaomba msamaha"
"ukishawaomba msamaha kula mtu akaridhika tena uwaambie kabisa nilikua nawapima tu imani... Alafu sasa wewe unaondoka zako na kuniacha mimi"
"Sitaki na sitaki"
"Ehh"
"hakuna cha Ehn sheby lazima tuondoke"
"sikiliza sasa.....  Ukishaondoka, mimi huku naanza vibweka bweka vya hapa na pale ili nifukuzwe kazi afu wakinifukuza tu... Moja kwa moja breki nyumbani kwako Dar es Salaam"
"mmmhhh kwa upendo huu kuna kufukuzwa kweli? ..... Mi sijui"
"kua na imani litawezekana... We ulifikili nitapataje kakitu kaliko vimba kama hako"
"ahahahahaha.. Jinga wewe unamuambia dada ako ivo wewe"
Kiukweli dada yobi alidata na mimi yaani alikufa akafia kabisa na sijui ni kwanini...  Basi tuliondoka sebuleni hapo yeye akaenda chumbani kwake na mimi nikaenda chumbani kwangu....
Kesho ndio siku dada yobi anaondoka zake kuelekea dar es Salaam, Hata mimi nilikua na shauku sana ya kwenda huko na natamani sana kwenda....

Leo ni siku nyingine tena ambayo ni Alhamisi, nililauka mapema sana na kuwapeleka akina asnati shuleni,..
"iv sheby, umedanganywa vipi na dada yobi uende dar?"
"Enhee hata mi namshangaa sana, yaani raha tunazokupa lakini bado huliziki sheby"
Walikua wakiniuliza kwa wote kua iv ni kweli naelekea huko, lakini mimi sikuwajibu kitu, nilikua bize na gari huku nikimuwaza dada yobi ambae ni dada yao na hawa akina asnati,
"we sheby si nakuuliza lakini mbona ivyo wewe"
Alikua ni Asnati ndio alioendelea kunisemesha,
"kwani nimeenda, mi nimekataa"
Niliwajibu hivyo huku nikiendelea kuendesha gari,..
Sauna aliposikia nimekataa alifurahi sana bila kujua kukataa huko ni kwasababu ya kuwaridhisha kwa siku mbili tatu hizi,..... Basi siku zilisonga na hatmae ule mwezi wangu wa kulipwa ulikaribia, na hapo ndipo nilipanza vituko ndani ya nyumba, yapata wiki moja sasa toka dada yobi aondoke,
"kijana wangu mbona siku hizi umebadirika kiasi hiki, yaani toka yobi aondoke umekua mtu wa tofauti sana, kwanini lakini kijana wangu"
Hayo yalikua ni malalamiko ya mzee huyo na yeye hataki niondoke maana kuna baadhi ya mirathi anataka kunirisisha, na hata katika moja ya mikataba yake ameisaini jina langu,..
"nipeni mshahara wangu, kila siku mi nagombana na mke wangu niache hii kazi lakini navumilia tu"
Ilikua ni mida ya usiku saa moja moja hivi, tukiwa sebuleni tukipata chakula, nilikua nimewaka mbaya yani nilikua staki utani hata kidogo,
Mara ghafla kwa bahati nzuri mke wangu kapiga simu muda huo huo, nami nikaiweka laudi spika ili na wao wasikie..
"haloo mke wangu habari yako mama"
"staki salamu yako, toka juzi unaniambia unaacha huo ujinga wako mbona mpaka leo hurudi... Mi nitaondoka naondoka"
"sikiliza basi mke wangu"
"sitaki endelea na hilo jim... "
Nilikata simu mana alikua anataka kusema endelea na hilo jimama lako, hivyo niliwahi kukata simu, mzee mwenyewe alikua kimya mama kashika shavu tu kwa mawazo mengi...
"ok, kijana naomba tuelekee nyumbani kwako ili tukaliweke sawa jambo hili, lakini sitaki uache kazi"
"mzeee suruhisho la kuokoa ndoa yangu ni kurudi kwangu tu, mana mke wangu kuna baadhi ya vitu kavigundua juu yangu hivyo hawezi kumuelewa mtu kabisa"
"nadhani mimi atanielewa hebu twende"
"mzee.... Naomba kuacha kazi"
Niliongea hivyo kisha nikawa naondoka kuelekea chumbani kwangu,
"mama yobi, mbona huongei upo kimya hivyo? Ataondoka huyu, utakesha kuleta vijana kila siku"
"muache aondoke tu"
Mama alikua hana mfupa wa kuongea sana kwasababu akiongea sana mzee anaweza kujua kua huenda kuna jambo lingine tofauti na kufanya kazi, na ni kweli jambo lipo na ndio lilionileta huku...

Siku kadhaa zilizopita na hatmae leo ndio siku ambayo nilikua nakabidhi ufunguo wao wa gari, ili niondoke kama nilivyokuja,
"yaani kijana wangu kweli unaondoka? Sawa sina jinsi mana siwezi kukulazimisha urithi usioutaka"
Sasa kumbe hili jambo la mzee kunirisisha mali zake mama halijui, sasa hapo ndio maskio yanamfunguka
"una maanisha nini baba yobi"
"ndio,... Mali zangu zote nilikua nampatia huyu kijana mana sina mtoto wa kiume"
"haaaaaa baba yobiiii jamani, wewe huna ndugu wewe"
"ninao"
"huna watoto wewe"
"ninao, ila ni wakike hawa wakiolewa na mali zote zimeolewa"
"haijalishi.... Kwahio kumbe kumbembeleza kote huko kumbe wataka umrisishe mali za wanangu.... Eeee baba sheby we nenda tu"
Mama sasa ndio akaamua kumalizia kunitimua kwa maneno baada ya kujua kua kumbe mumewe alikua anataka kuikosesha haki familia yake,
"sheby... Neeenda baba nimekuruhusu nenda"
Nilitika nikiwa naburuza zangu begi huku nikiwa nimelivaa lingine mgongoni, nilikua naelekea taarabu bila hata ya kuangalia nyuma, mana hata sipataki tena, Nilikua natembe huku nikiwaza nirudi kwa mke wangu au niende dar? Niliwaza lakini sikupata jibu sahihi... Sasa ile nakunja kona flani hivi, mara niliguswa bega, kugeuka kumbe alikua ni Sauna na dada yake nae ndio alikua anakuja ila alikua mbali kidogo...
"sheby, kweli unaondoka na kutuacha tukiwa wanyonge, lakini sitaki kukuficha kitu juu yangu... Umetembea na dada Asnati na mimi"
Nilimkatisha maongezi yake na kumwambia kua aongee Pointi mana nachelewa... 
"sheby... Ukweli ni kwamba, nina mimba yako"
"Uuu..   Uuu.. U. ..... U.. Uuuu....  Uuuu... Una.    Unasemaje Sauna"
"ndio, nina ujauzito wako"
Sasa huku nikiendelea kuumiza kichwa ili nijue ninafanyeje, mara ghafla Asnati kafika na kuanza kutapika mbele yangu namuona,..... Pale pale nae nikamuuliza shauku ya kujua ana nini, mana asije akaniambia na yeye ana mimba...
"Asnati?... Unaumwa na Maralia, Au ni Kaswende tu?... Sema basi unaumwa kaswende si ndio eee"
Nilikua natamani aseme hata kama anaumwa H.I.V kuliko aseme ana mimba,
"Bora ningeumwa hio kaswende au maralia kuliko ugonjwa nilionao"
"ugonjwa gani huo? Au ni gonorea"
"mbona unataja migonjwa yako tu siielewi,....Nina mimba yako"
"Tooobaaaa Yarabi Roho yangu mie, nitauweka wapi huu mwili"

Itaendelea..... after Tomorrow


KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU FANYA KUBOFYA LINK HII HAPA CHINI UKA LIKE PAGE ILI USIPITWE →→→↓↓↓

https://www.facebook.com/pages/Moon-vision-Enter/571095712946246?ref=hl

USIKOSE HAPO KESHOKUTWA USIKU... MIDA KAMA HIII HAPA

Share this

0 Comment to "MWIGIZAJI BALAYA Sehemu Ya 1"

Post a Comment