Sehemu Ya 1
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
SIMULIZI HII INAMHUSU KIJANA MMOJA AMBAE ALIISHI NA WAZAZI WAKE KATIKA MAISHA MAZURI NA YENYE FURAHA, LAKINI KADRI MAISHA YANAVYOZIDI KWENDA, NA WAZAZI WAKE NA HUPOTEZA MAISHA KAMA KAWAIDA, WAZAZI WALIACHA MALI NYINGI KWA AJILI YA MTOTO WAO HUYO MMOJA TU KAMA WA DAWA, LAKINI KUMBE NDUGU WA FAMILIA HIO HAWAKUA WAKIHITAJI UWEPO WA FAMILIA ILE IKIENDELEA KUISHI KWA FURAHA NA UPENDO, MTOTO YULE ALIZURUMIWA MALI ZILE NA NDUGU WA MAMA YAKE, YAANI BABA AU MAMA WADOGO WA UPANDE WA MAMA YAKE, MTOTO ALIISHI KWA SHIDA NA TABU KATIKA NYUMBA HIO, HUKU AKIWA KAMA MFANYAKAZI KATIKO NYUMBA HIO, NA MWISHO WA SIKU WALIAMUA KUMFUKUZA MTOTO YULE......
JE UNAJUA NINI KILIENDELEA BAADA YA KUFUKUZWA?..... USIKOSE HATA KIPANDE KIMOJA CHA SIMULIZI HIII.... ILA KAMA UNA ROHO NYEPESI USIISOME MAANA INASIKITISHA SANA,
TWENDE KAZI, NA HAPA NDIPO INAPOANZIA RASMI SIMULIZI HIII
Ikiwa ni mwaka 1999 nikiwa mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minne, maana nilizaliwa mwaka 1995, Nilikua nikitoka shule ya vidudu, almaarufu kama NURSARY SCHOOL, wazazi wangu walikua wakinipenda sana tena kwa uzuri ni kwamba nilikua nao wote, maisha kwetu yalikua ni mazuri kiasi kwamba baba alikua ana mkoko wake wa kutembelea, huku mama akifanya biashara ya kuuza nguo katika duka lake lililopo maeneo ya stendi jijini arusha, Kama kawaida mama yangu aliitwa MWAJABU na baba yangu aliitwa RASHIDY na mimi mwenyewe niliitwa SHARBINY au ukipenda niite SHEBY,..... Unaweza kujiuliza sana kwanini napenda kuyatumia hayo majina, ni kwasababu hayo ni majina ya wazazi wangu kabisa, yaani mbali na story zangu, basi hayo ni majina yao na sio ya kutungwa, na hilo jina la sharbiny ni lakwangu kabisa mimi muandishi wa simulizi hizi, hivyo usishangae kila story kuyasoma majina hayo, maana ni majina asilia na ya kweli kabisa......
Siku zilizidi kwenda na hatmae ni miaka mingi imepita mpaka nimemaliza shule ya msingi na sasa ndio naingia kuanza elimu yangu ya secondary kidato cha kwanza katika shule za international, maana wazazi wangu walijiweza kunilipia, maana baba yangu alikua akifanya kazi katika kampuni za kusafirisha wazungu, iitwayo LEOPARD COMPANY LTD ARUSHA kwahio kiukweli maisha yalikua sio mabaya sana,
"sheby?"
"yes dady"
"coming"
Niliitwa na baba yangu sebureni, na baba yangu alikua akiangalia mpira kwenye tv ilio kubwaa ya inchi 40,.... Kipindi hicho nilikua nina umri wa miaka kumi na nne (14), nilikua ni mtu mzima japo nilikua bado sijakomaa kiutu uzima, yaani kwa umri huo kama wewe unaakili basi nilikua bado ni mdogo sana kwani hata kubarehe yenyewe ilikua bado kabisa, na pia kutokana na malezi ambayo nimelelewa na familia yangu, basi ni ngumu sana kujua jua nambo ya kijinga jinga yasio na msingi wowote ule, kwani kawaida nikirudi tu shule hua nakimbilia madrasa au msikitini kusali..... Simulizi hiii inaendana kidooogo na ile ya SECONDARY SCHOOL ila hii ni balaaa, maana huko mbele mi sisemi ila ukiikosa mi simo
"yes dady"
"umerudi shule mwanangu"
"ndio baba, ila leo hujaleta zawadi dadiii"
"usijali, nitampigia mama yako simu akuletee chipsi kuku na kilo ya nyama, si utamaliza ee"
"ndio, tena nitakula afu sili usiku"
"mmmhhh mtoto muongo wewe, unaweza kumaliza kuku mzima na kilo ya nyama"
"vilete uone navipiga chap chap"
"sawa, tupinge usipomaliza sileti tena zawadi"
"haaaaaaaaa dadiiiii basi simalizi"
"uyoooo ahahahaha nilijua tu"
Nilikua nikifurahi na baba yangu mzazi kana kwamba tunaishi kwa amani na upendo tena kwa furaha ilio ya juu kuliko yeyote yule,.... Sasa we imagen upendo wa baba ni huo je huyo mama itakuaje, yaani ilikua ni familia ya kuigwa na watu wengine kupitia familia,
"vp unataka uangalie katuni zako"
"amna dadii mi nipo chumbani nafanya homework zangu"
"haya bwana"
Kwa upande wa shule kiukweli nilikua kichwa na ndoto zangu ni kuja kua dokta mkubwa katika tanzania hii, hio ndio ilikua ndoto yangu ya baadae,
Maisha yalikua ni mazuri sana juu yangu, kwani wazazi wangu wote walikuepo na walikua wakinipenda sana, maana nilikua nipo peke yangu katika familia yetu,...... Ila siku moja mamkubwa wangu alikuja kutusalimu huku mjini, akitokea kijijini, huyo ni mamkubwa kwa upande wa mama angu,.... Tulimpokea huku tukiwa na furaha juu ya ujio wake huo, ila siku moja nikiwa naenda msalani kujiseidia, usiku wa saa nane, nilishangaa kuona mtu kakaa nje kwenye kiti na usiku huo, hili lilikua ni jambo geni sana kwangu, niliwaza sana na kujua kua labda huenda akawa ni mama yangu anapunga upepo hapo nje, japo haikua tabia yake ya kupunga upepo mida hio, maana mama yangu anakaaga nje mwisho saa tatu usiku tena ni mpaka kuwe na mwezi ndio anatoka, sasa iweje leo aamke saa hizi,... Lakini nilipoangalia vizuri, ni kama hakua mwenyewe yaani walikua wapo kama watatu afu kuna mtu wamemzunguka katikati, na siku kwa bahati mbaya hakukua na umeme, walikua kama kuna kitu wanamfanyia huyu mtu waliomueka katikati, ila hakuna niliomuona sura kati yao,
Nilizidi kua na hofu huku nikinyata nyata ili niweze kuwasogelea karibu, lakini wazo langu lililopo kichwani ni kwamba, mimi najua ni baba na mama watakua wanacheza bao na jirani, hivyo nilikua nawamendea ili niwashtue, maana mama na baba wana tabia ya kucheza bao usiku, japo sio usiku mkubwa kama leo hiii, niliendelea kuinama huku nikijificha kwenye gadeni na maua yaliopo hapo, nilikua nahisi baridi sana, kwani nilitoka na boxer tu,...... Lakini nilipofika karibu nilishindwa kuelewa hawa wazazi wangu wanacheza bao gani, mbona sioni hata wakirusha rusha mikono zaidi ya kuona mikono ikiwa juu juu tu....... Nilijipa moyo kua huenda ni mchezo mpya waliougundua watu hawa, maana si wazee wa zamani hivyo watakua wakijua michezo mingi mno,..... Nilizidi kusogea mpaka nikakaribia karibu yao huku nikiwa nimejificha kwenye shina la ua moja kubwaaaa, lakini baridi ndio ilikua inanisumbua hivyo nikawa natetemeka sana huku, nikiwa nataka niwashtue baba na mama kama vile tunacheza kombolela,
Je? Unajua nini kitaendelea?
Itaendelea..... after Tomorrow
KWA STORY ZAIDI BOFYA HAPO CHINI KISHA UNGANA NASI KWA KUGONGA LIKE KWA HIO PAGE YETU →→→↓↓↓
https://www.facebook.com/pages/Moon-vision-Enter/571095712946246?ref=hl
USIKOSE HAPO KESHOKUTWA USIKU... MIDA KAMA HIII HAPA
0 Comment to "MTOTO WA HAYATI Sehemu Ya 1"
Post a Comment