Wednesday, May 9, 2018

WANAUME TU:- CHANZO NA TIBA YA KUFIKA KILELENI MAPEMA


CHANZO CHA MWANAUME KUFIKA KILELENI MAPEMA, NA TIBA YAKE

Matatizo ya kijinsia ni mengi  baadhi tunaweza kuyakabili kwa urahisi, na kuna mengine yanahitaji utaalamu maalumu kuyapatia tiba. Wakati mwingine maradhi husika huwa na taathira kutokana na mtu…. Na  tutazungumzia moja ya maradhi maarufu ya kijinsia… tutazungumzia tatizo la wanaume kuwahi kumwaga(PREMATURE EJACULATION).


Premature Ejaculation  ni hali ya mwanaume kuwahi kufika kileleni ndani ya sekunde 30 hadi dakika nne baada ya kuanza tendo.
 Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, tatizo la kuwahi kumwaga (Premature Ejaculation) ni miongoni mwa matatizo ya kijinsia yaliyoenea sana kwa wanaume, na ni mzigo mkubwa wa kisaikolojia kwa mume. Aidha, tatizo hilo humfanya mwanamke achanganyikiwe na hata kumfanya asiwe na hamu kubwa ya kushiriki tendo au kulikimbia tendo la ndoa kwa hofu ya kutotoshelezwa.
Tafiti zinaonesha kuwa asilimia kubwa ya vijana wapya katika ndoa hukabiliwa na tatizo la kumwaga mapema, na huwenda tatizo hilo likaendelea kwa miaka mingi.
Tatizo hili ambalo hujitokeza dakika moja kabla ya mwanaume kumuingilia mwanamke au dakika moja baada ya kumuingilia, humfanya mwanaume asiwe na uwezo wa kuchelewa kumwaga.
Maradhi haya hutokana na taathira hasi za kisaikolojia na kijamii kwa mwanaume husika, kama vile wasiwasi na mkanganyiko, na linaweza kumfanya akimbie kushiriki tendo la ndoa.

 Kwa mujibu wa tafiti na ripoti mbalimbali, maradhi haya ndiyo maradhi yaliyoenea zaidi miongoni mwa maradhi ya udhaifu wa kiume, ambapo inakadiriwa kuwa asilimia 39 ya wanaume wenye umri kati ya miaka 18 na 64 wanasumbuliwa nao. Tofauti na maradhi mengine ya udhaifu wa kijinsia (kama vile tatizo la kusimamisha), tatizo hili halina uhusiano na umri wa mhusika.

SABABU ZA KUWAHI KUFIKA KILELENI MAPEMA

 Kuna sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo. Kuna sababu za kurithi, sababu za kimwili na sababu za kisaikolojia. Miongoni mwa sababu za kimwili ni pamoja na kutokea kwa kasoro katika homoni muhimu ya kiume ijulikanayo kama “testosterone”, au athari za matumizi ya baadhi ya dawa, kama vile dawa za kupunguza shinikizo la damu, au kutokana na kuacha matumizi ya dawa za matatizo ya kisaikolojia na kiakili. Na huwenda sababu ikawa ni ongezeko la utoaji wa tezi thioridi (asilimia 50 ya wanaume wenye kusumbuliwa na tezi thioridi wanasumbuliwa na tatizo la kuwahi kumwaga), au kibofu sugu (asilimia 77 ya wanaume wenye tatizo la kibofu sugu wanasumbuliwa na tatizo la kuwahi kumwaga).

Miongoni mwa sababu za kisaikolojia ni pamoja na fadhaiko, wasiwasi uliopitiliza kuhusu uwezo wa kufanya tendo la ndoa, au dhulma za kijinsia ambazo alikumbana nazo utotoni mwake.

ATHARI ZA KUWAHI KUFIKA KILELENI MAPEMA

 Athari ya tatizo la kuwahi kumwaga hutokana na athari zake, ambazo zinamsibu mwanaume na mwanamke kwa pamoja. Miongoni mwa athari mbaya za maradhi haya ni mhusika kujihisi uduni na kutouamini uwezo wake wa kiume. Baadhi wa wanaume, wanaweza kukatisha uhusiano wa ndoa au kutengeneza matatizo ili kuepuka hisia za kushindwa.

Tatizo hili linaweza pia kumzuia kijana kuingia kwenye ndoa. Aidha, huibua wasiwasi na hofu ambayo huonekana katika muamala wake sio tu na mkewe, bali pia muamala wake kwa watu wanaomzunguka.

Ama kwa upande wa mke, atahisi hali ya kukanganyikiwa na kuhisi kwamba ametengwa kwa sababu ya hatua za mume zisizokuwa za kawaida za kujitenga na mkewe. 
Pia inaweza kumfanya mke asijiamini na kuhisi kuwa mumewe anamtenga kwa sababu anavutiwa na mwanamke mwingine.
 Kuna utafiti unaoonesha kuwa pindi mume anapokuwa na tatizo la udhaifu wa kiume basi asilimia 42 ya wanawake huhisi kuwa wao ndio tatizo, yaani wanahisi kuwa tatizo hilo la mume linatokana na wao kutokuwa na mvuto kwa waume zao.

TIBA YA KUWAHI KUFIKA KILELENI MAPEMA

Baada ya kujua sababu, hatari na athari za maradhi hayo, hatuna budi tujue tiba na dawa ambazo tunaweza kuzitumia kuondoa tatizo hilo la kumwaga mapema. Njia za kuondokana na tatizo hilo zimegawanyika katika maeneo 3 kutokana na chanzo chake:

Kwanza unapokuwa ukishiriki tendo jitahidi kufanya taratibu usiwe na papara, Wengi wamejikuta wakiwa na shida hii kutokana na kuwa na papara au haraka katikati ya tendo na hali hiyo wengi hujifunza kupitia mikanda ya ngono wakidhani kuwa kulala na mwanamke ni lazima ufanye kwa haraka ndio uonekane mwanaume kweli. Lakini ukweli ni kwamba unapofanya taratibu ni njia nzuri zaidi kwani utamfikisha mwenzi wako na wewe utachelewa kufika kilele pia.  

1.NJIA YA KISAIKOLOJIA: 

Hapa kinachotakiwa kuangaliwa ni yale matatizo ya ndoa. Mke anaweza kuzungumza na mume kumuondolea wasiwasi na kutafuta njia za kuyashughulikia matatizo yao. Pia, mume anatakiwa kutokuwa na wasiwasi kuhusu uwezo wake wa kiume.Ni muhimu utambue uwezo wa mwanaume kushiriki tendo la ndoa huanzia kwenye akili yake. Bila utulivu wa kiakili sahau kuhusu utendaji mzuri kitandani.

2.KUTUMIA MBINU: 

Njia hii inasaidia kuboresha uwezo wa mwanaume katika kudhibiti umwagaji kwa kutumia baadhi ya mbinu maalumu. Kwa mfano, wakati anapokaribia kumwaga anaweza kuchomoa dhakari yake na kuanza upya au kutulia kwa sekunde 30 alafu akaendelea. Pia anaweza kutumia mbinu ya kuiminya dhakari yake.Yaani  Jenga utaratibu wa Fanya na kuacha: hii ni ile hali ya unapoona unakaribia kutoa mbegu basi unaweza kusimama angalau kwa sekundi 30 kisha unaanza upya. Hii husaidia sana kuchelewa kufika kileleni na hauta weza kumaliza kwa haraka.

3.DAWA : 

Ama kuhusu dawa, kuna dawa fulani iliyopitishwa hivi  inaitwa Lejam. Dawa hii inasaidia kutatua tatizo la kuwahi kumwaga.Pia dawa kama Tramadol japo ni dawa ya maumivu ila tafiti zinaonesha kuwa inaweza kuchelewesha mtu kufika kileleni hivyo kutumika pia kutibu tatizo hili.
Mwisho matumizi ya Condom pia huweza kumfanya mtu kuchelewa kufika kilelen

Ila tiba kuu zaidi ni kufanya mazoezi kwa wingi na kukontroo hisia zako kisaikolojia...

USIKOSE MAKALA NYINGINE HAPO KESHO UKIWA NAMI 

Dr Voice Mgosi
+255714419487 WhatsApp 

KAMA WEWE NI MPENZI WA LOVE STORY, MAMBO YA CHOMBEZO ZA HUBA, MAHABA, MKATABA, MARAHABAAAA, NA HAPA NDIO KWAO

UNAPITWAJE NA UTAMU HUU? 

ORODHA YA STORI ZANGU ZOTE HII HAPA, NI BUUURE BONYEZA HAPA

www.moonvisioner.blogspot.in/search/label/CHOMBEZO

(1).KIJAKAZI WA KIUME

(2).MLINZI WA GETI

(3).DEREVA TOYO

(4).MTOTO WA HAYATI

(5).ONE DAY YES

(6).SECONDARY SCHOOL

(7).FUNDI CHEREHANI

(8).MWIGIZAJI BALAYA

(9).THE DOM

(10).THE ISLAMIC WIFE

(11).MKE JEURI

(12).YOUNG PASTOR

(13).MUUZA CHIPSI

HIZO ZOTE, INGIA GOOGLE TAFUTA ULIO IPENDA, AU BONYEZA HAPA CHINI, UKAZISOME ZOTE, BUUURE

www.moonvisioner.blogspot.in/search/label/CHOMBEZO

AU.... Njoo WhatsApp Ujipimie....

Utazipata Zote Mpaka Mwisho Kwa Simu No: +255714419487 WhatsApp, Au, Like Page Yetu Ya Facebook Iitwayo CHOMBEZO MEDIA

tAfBoy {.Tanzania's Frugal Boy..}

Share this

0 Comment to "WANAUME TU:- CHANZO NA TIBA YA KUFIKA KILELENI MAPEMA"

Post a Comment