Sunday, May 27, 2018

DALILI KWAMBA MWANAO ANAHARIBIWA KIMAUMBILE




DALILI 11 ZA MTOTO WA KIUME ALIE ANZA KULAWITIWA NA WENZIE

Baada ya televisheni ya Clouds kurusha kipindi kuhusu ushoga watu wengi wamekuwa wakilalamika katika mitando ya kijamii na kuonyesha hisia zao kuchukia tendo hilo.

Ni tendo baya ambalo limelaaniwa na vitabu vya Mwenyezi Mungu, lakini haya yanatokeaje? 

Inafikiaje mpaka mwanaume kukubali kuingiliwa na mwanaume mwingine

Jambo hili halitokei mara moja tu kwa maana kwamba mtu hakai tu akaamua kuwa leo nakuwa Shoga anaanzia mbali.

Mashoga wengi unaowaona leo wamenza kipindi wakiwa watoto, wamekua hivyo na sasa wanaona ni kitu cha kawaida.

Lakini wakati wanaanza wazazi wao walikuwa wapi? 

Nani aliwafundisha mchezo huo na ni kwa namna gani wewe kama mzazi utagundua mapema kuwa mwanao anajihusisha na mambo hayo na kumsaidia kabla ya kuharibikiwa ???

Baada ya kuona kelele nyingi nimeona nichambue baadhi ya dalili kuu ambazo ukianza kuziona kwa mwanao inabidi uanze kumchunguza kwani kuna tatizo.

Kama wewe ni mzazi, mlezi, ni kaka, ni dada, shangazi au mjomba unalo jukumu la kuhakikisha mtoto wako yuko salama.

Usiishie kulalamika na kutukana katika mitandao wakati kuna mtu anamharibu mwanao.

Kwa kiasi kikubwa watoto wengi huharibiwa na watu wao wakaribu, wanaweza kuwa watoto wenzao wakubwa kidogo, wanaweza kuwa ndugu au walimu hivyo kama ukiona dalili hizo hapo chini kwa mwanao bila kujali jinsia yake basi jua kuna kitu kinaendelea chunguza.

(1) GHAFLA ANABADILIKA TABIA

anakuwa muoga, mwenye msongo wa mawazo, hataki kurudi nyumbani au kwenda sehemu flani, au anaanza kumuogopa mtu flani, hata akisikia jina lake tu anastuka.

(2) MANENO MAZITO

Anaanza kuongea maneno makubwa kuliko umri wake hasa ya mambo ya kimapenzi, akiwa na watoto wenzake anawafundisha vitu vya hovyo au unasikia akitamka maneno ambayo ni ya kikubwa.

(3) MFUMO WA KULALA

Anabadilisha mfumo wa kulala, kila akilala ni kustuka stuka kana kwamba anaota anaweza hata kupiga kelele, ngumu sana kupata usingizi na anaonekana kuchoka sana mara kwa mara.

(4) KULA SANA WAKATI SIO KAWAIDA YAKE

Ghafla anaanza kula sana mpaka unakuta anaanza kuongezeka uzito kwa kasi, inawezekana ni kutokana na stress anahamishia stress zake katika chakula.

(5) MABADILIKO YA KUKAA AU KUTEMBEA 

Anapata shida wakati wa kukaa au kutembea, unamuona kabisa anakunja uso wakati wa kukaa au hutembea kwa kuchechemea.

(6) MIKWARUZO 

Mikwaruzo kwaruzo katika sehemu mbalimbali za mwili wake ambayo haielezeki na ukimuuliza hana majibu ya uhakika anaweza hata kuanza kulia kwa uoga.

(7) MUONGO

Ghafla anaanza kuwa muongo muongo kuhusu sehemu ambayo alikuwepo, humuoni nyumbani kwa muda na ukimuuliza ulikuwa wapi anadanganya bila sababu.

(8) TABIA ZA KITOTO KULIKO UMRI WAKE 

Anaonyesha tabia za kitoto kuliko umri wake bila sababu, mfano anaanza kukojoa kitandani wakati alishaacha, kulialia na kujificha ficha kila akiona watu au kukasirika kasirika bila sababu.

Mzazi ukikutana na dalili hizo jaribu kuonge ana mwanao, usiongee kwa ukali kwani mtu ambaye anamfanyia hivyo tayari alishamtisha na yeye kama mtoto anajua kuwa hawezi kuaminika hasa kama mtu anayemfanyia ni mwanafamilia wa karibu ambaye anaheshimika.

Onyesha kuwa unamuamini hata kama kitu anachokuambia kinaonekana hakileti maana kwa wakati huo.

Tujitahidi sana kuwa na tabia ya kuwapeleka au kuwafua wanao Shuleni mara kwa mara kwa kushtukiza, bila taarifa au ratiba maalum, hata kama wana School Bus ya kuwafata na kuwapeleka Shuleni

Tuepuke sana kuwapeleka watoto wadogo Boarding School, watoto wengi huanzia hizi tabia huko.

Share post hii kwa wengine inawezekana angalau mtoto mmoja unaweza kumuokoa, tuache tu kulalamika tifanye kitu.

USIKOSE MAKALA NYINGINE HAPO KESHO UKIWA NAMI 

Dr Voice Mgosi
+255714419487 WhatsApp 

KAMA WEWE NI MPENZI WA LOVE STORY, MAMBO YA CHOMBEZO ZA HUBA, MAHABA, MKATABA, MARAHABAAAA, NA HAPA NDIO KWAO

UNAPITWAJE NA UTAMU HUU? 

ORODHA YA STORI ZANGU ZOTE HII HAPA, NI BUUURE BONYEZA HAPA

www.moonvisioner.blogspot.in/search/label/CHOMBEZO

(1).KIJAKAZI WA KIUME

(2).MLINZI WA GETI

(3).DEREVA TOYO

(4).MTOTO WA HAYATI

(5).ONE DAY YES

(6).SECONDARY SCHOOL

(7).FUNDI CHEREHANI

(8).MWIGIZAJI BALAYA

(9).THE DOM

(10).THE ISLAMIC WIFE

(11).MKE JEURI

(12).YOUNG PASTOR

(13).MUUZA CHIPSI

HIZO ZOTE, INGIA GOOGLE TAFUTA ULIO IPENDA, AU BONYEZA HAPA CHINI, UKAZISOME ZOTE, BUUURE

www.moonvisioner.blogspot.in/search/label/CHOMBEZO

AU.... Njoo WhatsApp Ujipimie....

Utazipata Zote Mpaka Mwisho Kwa Simu No: +255714419487 WhatsApp, Au, Like Page Yetu Ya Facebook Iitwayo CHOMBEZO MEDIA

tAfBoy {.Tanzania's Frugal Boy..}

Share this

0 Comment to "DALILI KWAMBA MWANAO ANAHARIBIWA KIMAUMBILE "

Post a Comment