CHOZI LA MAMA YANGU
(Masharti Ya Jini Maimuna)
Sehemu Ya........
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/
Ilipoishia Jana...
"naona bora na mimi nife mama, sina raha na huu mji... Kila mtu ananitenga"
"nyamaza mwanangu.... Hebu angalia hii hali tulio nayo kwa sasa,.. Baba yako ndio huyo hana kazi, mimi ndio kama unavyo niona, tegemeo letu ni wewe, leo unalia ivi unadhani nasi tunajisikiaje..."
"mama,sina hamu ya kuishi kabisa, kama surian nimemuua mimi, basi bora na mimi nimfuate huko huko"
"ashaaaaaaa.... Wewe ni mshenzi,... Sitaki kusikia huu upuuzi mimi... Hebu amka uenda saluni tupate chochote"
Aliongea mama yake asha,.. Mana anamfokea huku akimpoza
"mama.... Saluni nilisha iuaza yote... Mana pesa niliokua napata awali, Kiukweli kwa sasa inachosha sana... Nimesha uza kila kitu"
"haaaaaaaaa.... Asha mwanangu... Sasa tutakula nini?... Kwanini lakini umeuza? Hata kama ni mali yako, lakini ilikuwa ikitusaidia"
Aliongea mama yake asha, lakini wakiwa bado wanazungumza... Ghafla mlango ulisukumwa....
"heeeeeeeeeeeeeeeee"
Mama alitahamaki kana kwamba kuna mtu kaingia bila kutarajia
ENDELEA..........
Hakuna kitu kibaya katika hii dunia kama kuzushiwa jambo ambalo hujalifanya, hususan kwenye upande wa kifo,... Asha anaye nyooshewa vidole kwa taarifa za kumuua ndugu yake surian kisa ni pesa, na ukiangalia ni kama kweli, mana wakati surian anapotea, huku nyuma asha kaanza kupiga pesa kupitia pete aliokuwa kaivaa, japo mpaka leo hajui kuwa pete ile ndio sababu ya biashara yake kuwa nzuri,...
Mpaka sasa asha keshauza saluni yake yote kwani ndio sababu ya kunyooshewa vidole na watu juu ya ndugu yake. Mama yake alilaani sana kwa kitendo cha asha kuuza saluni yote ili kupunguza lawama ya kwamba saluni ile ndipo mdogo wake alipo pale,.. Mana asha alipiga pesa mpaka akanunua uwanja na kujenga Nyumba ambayo kwa sasa ipo kwenye lenta,... Na hapo ndipo ilipo ishia,... Maisha yao toka kuzaliwa kwake wameishi kwenye kota za serikali, hivyo akaona bora ajenge,.. Sasa katulia tu nyumbani ni mtu wa kulia...
Lakini wakiwa bado wanazungumza... Ghafla mlango ulisukumwa....
"heeeeeeeeeeeeeeeee"
Mama alitahamaki kana kwamba kuna mtu kaingia bila kutarajia....
"Heeeeeeee, baba asha haya nini tena, au wakimbizwa huko nje"
Aliuliza mama asha, kumbe alio ingia kwa haraka hivyo ni mzew Rashidi ambaye ni baba yake surian au asha.
"hapana mke wangu,... Kuna tangazo la kazi nimeliona na kesho ndio wanafanya usaili,... Sasa nimeona nimuwahishie asha akajaribu kazi pale, mana hapa wameandika wanataka wanaume 200 (miambili) na wanawake 300 (Miatatu)... Natamani kwenda, lakini kama mnavyojua mimi ni mbovu wa kifua, hivyo kazi za viwandani siziwezi... Asha mwangu, hebu kajaribu ili tupate chochote mama"
Baba yake asha kumbe alikimbiza tangazo la kazi, ili asha ajiandae mapema, mana kesho ndio usaili (uchambuzi wa wafanyakazi)... Hivyo kawahi kumpelekea mana yeye ndio alikuwa mitaani huko...
"baba, Utanisamehe sana... Kwa sasa sitaki kazi"
Asha alikataa kupokea wito wa baba yake... Na yote hio ni hasira...
"asha, unamkatalia baba yako"
Mama aliingilia kati huku baba akisema kuwa
"asha, hawahitaji vitu vingi, wanataka barua ya maombi ya kazi na vyeti vya shule tu"
"baba na mama.... Mmeshindwa kunisomesha vizuri nipate kazi nzuri... Leo mnaniletea kazi zinazo tangazwa mitaani... Mimi sitaki, msubirini msomi wenu aje mumpe hilo tangazo"
Asha aliwajibu wazazi wake hivyo huku akiondoka kwa hasira kali,...
baba yake kuna kaulia alitaka kuitoa kama kumuachia laana kutokana na majibu yake lakini mama akamzuia mume wake asiongee lolote, kwani asha hapo alipo ana hasira sana kwa kashfa anayo pewa....
"mama asha, hivi hapa tumezaa au tumemuokota huyu mtoto"
"baba asha, huko unafika mbali sasa, ukumhuke huyu mtoto ana hasira kutokana na kashfa anayo pewa mitaani"
"hata kama ana kashfa, haya sio majibu ya kutujibu sisi... Tumemkosea nini... Kufeli kwake ndio sababu ya kutulaumu kuwa hatujamsomesha... Mbona anataka kuniliza huyu mtoto"
Aliongea mzew Rashidi huku akitaka hata kulia lakini mama anazuia machozi yasimtoke mzee Rashidi, kwani yakitoka ni laana kwa asha, mana kasababisha mzazi kalia kwa ajili yake... Hivyo mama alifanikiwa kuzuia machozi ya mume wake... Walikaa mahali yeye na mke wake wakiwa wanatulizana kama mke na mume....
"sasa mama asha... Mimi naona niandike barua tu... Angalao nikawe hata dereva"
Aliongea baba yake suria kuwa aandike barua akaombe kazi ya udereva
"baba asha, hivi unaongea nini"
"mama asha... Tulikua tukimtegemea mwenetu asha, leo asha hana kitu, tutakula nini humu ndani... Wacha niende nikaombe udereva, mana wana pia wanahitajika madereva"
Aliongea baba yake asha huku akitoka kwenda kununua karatasi ili aandike barua ya kazi...
"heeeee baba asha... Huo udereva ulijifunza lini? Au wataka ukafe huko kama mtoto wako suria alivyokufa... Hebu niachie hilo balaa... Wacha mimi nitakwenda, we niandike barua ya maombi ya kazi"
Mama aliona ni bora aende akaombe kazi yeye kuliko mume wake, kwani hawezi udereva ila anataka kwenda tu, kuachilia hawezi pia anaumwa na kifua kwa miaka mingi, hivyo i Afadhali ya mama kidogo ana kajinguvu ka kufanya kazi
"mke wangu... Ina maana wewe ufanye kazi mimi nile"
"baba asha... Mbona uko hivyo... Mimi nimekula vyako vingapi, sembuse mshahara wangu?"
"mmmhhh sawa, lakini nitakuwa nakusindikiza mpaka getini, na kuja kukuchukua"
Aliongea baba yake suria huku akicheka
"kwanini sasa ufanye hivyo"
"heeee... Si namlinda mke wangu"
"hehehehehe yaani baba asha wewe hukui, sasa na uzee huu nani anifuata"
"weeeeeeeeeee.... Heeee we sema hivyo tu, mi ndio najua siri ilioko hapo"
Aliongea mzee rashidi huku akitoka kwenda kununua karatasi ya barua, ili amuandikie mkewe barua ya kazi... Sasa mzee Rashidi ana wivu mana mama yake suria anazeheka nalo...
Tukija huku dukani kwa faima
"sasa umerudi kazini, chezea tena..."
Aliongea zamina dada yake na faima akiwa dukani anapouza mdogo wake
"dada, mimi nakuelewa ila Kiukweli suria hatoki kichwani mwangu,.. Sijui kama huko alipo kama ananisikia"
Aliongea faima huku zamina akisema
"wewe acha ujinga, suria, suria kila siku suria... Mtu keshauwawa na dada yake wewe unateseka tu"
Mara zamina alitulia kwani simu yake iliita...
"halo shem mambo"
Alipokea simu hio huku akisema shem, lakini sauti ya huyo shem haikusikika
"eeeh umefika"
Aliongea faima kana kwamba huyo shem yupo maeneo hayo...
"ok njoo kwenye duka moja hivi, ulizia IC (ISLAMIC CLOTH) ndipo nilipo"
Alimuelekeza mtu huyo
"umepaona eee?"
Alijibu mwenyewe kisha akamalizia kusema
"sawa njoo chap basi"
Zamina alikata simu kisha akamwambia mdogo wake kuwa
"acha na wanaume wasio na mbele wala nyuma... Tariki unamkataa bure tu lakini ana hela, acha ufala.. Na ndio huyo anakuja, ongea nae vizuri"
Aliongea zamina kisha akaamka pale kwenye kiti,.. Alikuja jamaa mmoja sharobaro mno, na pia alionekana kuwa nazo kutokana na nguo kali alizo vaa...
"ooohhh shem Riki, mambo"
"poa shem nambie"
"safi tu... Kumbe we mwenyeji hapa IC?"
"ndio, mbona ndio mitaa yetu hii"
"wacha Weeeee"
"ndio"
"ok karibu,.. Mwenzio uyo apo.... Sasa faima mi naenda kwa tizo"
"sawa dada"
Zamina aliondoka zake hivyo faima akabaki na Tariki, ikiwa wateja wamepungua kidogo....
"mambo fai?"
Tariki alimsalimia faima, lakini faima hakuwa na muda nae tena anatamani wateja waje ili asiongee na Riki....
"nakusalimia tu jamani fai"
"shida yako nini riki,.. Sitaki kuongea na wewe"
"lakini fai,... Moyo ndio unanipeleka puta juu yako,.. Mimi ni mtu na pesa zangu, inakuwaje nakosa mtu wa kutumia nae"
Aliongea Tariki, huku faima ndio kwanza hata habari hana....
"pesa ni zako na familia yako, hazinihusu hizo"
"fai ina maana bado unampenda mtu aliokufa.... Umekuwa mkali mpaka nimeamua kumtumia dada yako"
"tariki tafadhali sana naomba usinichefue"
Faima alimjibu tariki huku tariki akituma sms kwa zamina mana ndio msaada wake...
Ghafla simu ya faima inaita.. Kucheki ni dada yake...
"halloo"
Aliipokea faima na kuita haloo"
"acha ujinga wewe, kupenda gani huko mpaka kwa watu waliokufa... Acha ujinga, wanaume siku hizi hakuna sasa potezea hio bahati endelea kupenda mtu aliokufa, na ukumhuke umri wako unazidi kwenda na utahitaji ndoa.. Sasa jifanye unapenda utaolewa na mizimu ya suria"
Aliongea zamina kisha akakata simu
Faima alihema kwa nguvu kisha akamuangalia tariki...
"naomba uondoke na staki uje tena"
"nini tena faima"
"nasema tokaaa"
"ok poa, ila siku ukijiskia... Utanicheki kwenye simu, namba yangu hio hapo"
Tariki aliacha karatasi yenye namba za simu yake, ili siku faima akifikiria vyema basi amtafute kwa namba hio
Hivyo tariki aliondoka zake, lakini alipofika mahali alikutana na rafiki yake wa kiume ambaye alikuja naye lakini hakutaka afike nae pale IC, hivyo alimuacha mbali na hata rafiki huyo anajua leongo la tariki...
"riki vipi"
Aliuliza rafiki yake huyo, huku riki akijibu
"mmmhhh ebana mtoto ni mgumu... Nimejigamba nina hela lakini wapi mtoto hajali wala nini"
Aliongea tariki, kana kwamba hana pesa wala nini sema ilikuwa mikwara ya kutongozea tu....
"unajua tariki unakosea,.. Na ndio mana mademu hukai nao... Mana unajinadi sana kuwa na pesa wakati hata kazi huna"
"sasa jumbe kama unavyojua, mademu wa sasa hivi ni wakali kinoma ila kuwapata ni mkwanja, ukumhuke samaki bila chambo humpati ujue"
"ni sawa, lakini kumbuka yule sio samaki"
"wacha nijitape tu... Akichomoa poa kwani kwsho si tunakwenda kupata kazi kule kiwandani"
"na usipo pata je"
"fresh tuuu"
"afu sitaki kuamini kuwa hata dada yake anajua una hela"
"sasa je? Anajua ninazo... We ulizani kwa pamba hizi ataachaje kuamini"
"duuuuuu, yaani wewe ni zaidi ya Jambazi aiseee"
Tukiachana na hao tuje huku kwa akina surian na mke wake maimuna waliokuwa ofisini, na msichana mmoja hivi ambae yeye ni jirani yao, baada ya kuskia anatafuta kazi,... Na dada huyo alisomea usekretari, hivyo imekuwa rahisi sana kwake kupata kazi,... Wakiwa hapo ofisini dada alianza kuonyeshwa sehemu yake ya kazi,...
"sasa wewe ndio sekretari wa kampuni hii, haruhusiwi mtu yeyote kumuona boss bila wewe kuleta taarifa zake kwangu"
Aliongea surian na hapo alikuwa na mke wake maimuna,
"sawa boss, nitafanya kazi kadri ya uwezo wangu ni sitakiuka kanuni na taratibu za kampuni hii"
"ok... Nadhani kwa siku ya kesho utapata changamoto kubwa na kazi kubwa pia kwasababu kwsho ndio siku ya usaili, hivyo wataingia watu watano watano, utamkagua mmoja baada ya mwingine kisha unaniletea barua yake ikiwa na vyeti vyake... Nitakapo ona vyeti ya mhusika, basi mimi ndio nitajua namuweka nafasi gani kitokana na elimu yake"
"sawa boss,. Naaa... Mfanyakazi anaruhusiwa kuingia ofisini kwako"
"hapana... Haruhusiwi mtu yeyote kuingia ofisini kwangu, ispokuwa wewe na mke wangu tu... Hivyo ofisi itaingiliwa na watu watatu... MIMI NA MKE WANGU PAMOJA NA WEWE na wewe utaingia kwa kuleta document au taarifa za kitu au mtu fulani, sio kuingia mara kwa mara kwakua unaruhusiwa, na hata awe boss wa kampuni gani, mwambie anisubiri chumba cha meeting (mikutano)... Nadhani umenielewa"
"nimekuelewa boss... Hivyo kesho, nakagua barua za mtu kisha nakuletea"
"yes, na uhakikishe barua imekamilika vigezo vyote ndio uilete kwangu kama naipitisha au laa, na kama haijakamilika sitaki usumbufu, mtu huyo arudi akakamilishe vigezo vyote... Sawa Cecilia"
"sawa boss"
"ok, nipo ofisini kwa wale watakao tokea leo wapokee tu"
"sawa boss"
Ilikuwa ni mipango ya kazi ambayo anatakiwa kufanya sekretari huyo, ikiwa ni kampuni mpya katika mkoa wa tanga, na inahitaji watu takribani 500 (miatano) ikiwa na lengo la kusaidia watu kwa njia ya kuwaajiri, kampuni ya MOON ISLAMIC CLOTH COMPANY, Ipo tayari kwa wafanyakazi kuleta maombi ya kazi
Kesho yake asubuhi mida ya saa mbili, ndani ya geti la kampuni hio kulifulika watu wengi mithili ya soko, kweli hapo kazi ipo... Watu walikuwa ni wengi mno na uchambuzi huu hautakiwi kufanywa na maimati, mana yeye hutumia nguvu za asili yake, hivyo asije kupitisha watu Ilimradi tu......
Katikati ya watu zaidi ya miambili alionekana mama yake surian akiwa kashika bahasha yake, naye kaja kuomba kazi kwenye kampuni hio, na watu woote walikuwa na umri usiopungua miaka 18 mpaka 35 lakini mama kajikaza tu kuka mana haoni lika lake kati ya wafanyakazi aliosimama nao... Mama suria au mama asha anachungulia tu kama angalao hata atamuona boss ampe kipaumbele kwakua ni mtu mzima,.. Lakini kwa bahati mbaya au nzuri boss keshaingia ndani na haruhusiwi kutoka wala kuingia mtu...
"heeee we mama vipi mbona unanisukuma"
Aliongea dada mmoja huku kama wakimcheka mama yakw suria,.. Yaani laini wangelijua kuwa huyo ndio mama wa bosa wanaye muomba kazi sijui ingelikuwaje, na mama nae hajui kama anakwenda kuomba kazi kwenye kampuni anayomiliki mtoto wake, na hata mtoto hajui kuwa mama yake kaja kuomba kazi,...
Usaili Ulianza, na vigozo visipo timia unarudishwa ukatimize vigezo, na kama huezi basi usirudi tena... Hivyo kuna wale ambao hawana vigezo basi wanarudi lakini namba zao zimeachwa kwamba watachukuliwa kama masalia tu... Hivyo hata akiondoka namba inaachwa kwa sekretari, siku akihitajika mtu aitwe...
Wasichana walikuwa wakimcheka mama asha, kwani alikuwa na umri mkubwa sana
"huyu mama jamani ananikanyaga"
"we mama ulikuwa wapi ujanani kwako"
Walikuwa ni wasichana waliokosa heshima ndio walikuwa wakimsema mama huyo, mpaka mama asha akakata tamaa na kukaa pembeni mana alikuwa kwenye nafasi ya kuitwa lakini akajikuta karudi nyuma ili asichekwe na watoto kulingana na umri wake..
Pamoja na uvumilivu wake wote, zamu yake ilifika akiwa na furaha kwa kupata nafasi, wengine walicheka sana... Na hata sekretari alishtuka kumuona mama mwenye umri mkubwa amekuja kuomba kazi za viwandani...
"heeeee mama.... Hata wewe"
Alikuwa sekretari ndio mwenye kuongea
"ndio mwanangu, nitafanya kazi usinione hivi tuuu"
Aliongea mama asha au mama surian na mama huyu anasikia tu mtoto wake kafa lakini hana imani hio mana yapata miezi miwili hamjui alipo wala hajawahi kuwasiliana nae
"mama, umri wako hauruhusu kufanya kazi hapa... Na hata karatasi ya matangazo ilisema ni kuanzia miaka 18 mpaka 35 ndio mwisho... Kwani mama una umri gani"
Aliuliza sekretari huyo huku mama akiwa mshapu kujibu ili aonekane yupo shapu hata kwa kufanya kazi
"nina miaka 58"
"haaaaaaaaaa mama, haiwezekani"
"jamani nipeni hata kufagia fagia tu"
"labda ingekuwa hio lakini hata vyeti vya shule huna, hapa naona barua na paspoti saizi tu"
Aliongea Cecilia huku akisoma barua ya mama huyo
"nisaidie mwanangu... Ina mana nife njaa na nina uwezo hata wa kudeki vyoo"
"mama, tatizo ni umri wako ni mkubwa sana... Kwani huna watoto wasomi waje tuwape nafasi"
Aliongea Cecilia bila kujua boss wake ndio mtoto wa huyo mama lakini hakuna anaejua hilo... Sasa Cecilia aliposema hivyo, mama akakumbuka mtoto suria ambaye ni msomi mpaka basi,....
"usinikumbushe yaliopita mwanangu, nisaidie kazi"
"mama, kweli naogopa kufokewa na boss kama nitaipeleka hii barua"
"jaribu tu, nitasafisha hata vyoo tu"
"mmhhh mama angu unanipa mtihani"
Mara ghafla simu ya mezani kwa Cecilia inaita... Alipokea
"hallo boss"
"eeehh vipi watu wameisha??"
"hapana boss bado wapo"
"sasa mbona huleti document zao"
"naleta boss.. Ila kuna"
Cecilia alitaka kusema lakini akasita,.. Sasa alipomwangalia yule mama anatia huruma sana
"ila nini ceci? Lete document muda unakwenda huu"
"boss?"
"nini Cecilia? Lete"
"boss... Kuna mama mtu mzima hapa, hana vyeti, ana miaka 58..je tunamsaidiaje"
Aliongea Cecilia, huku akisubiri jibu toka kwa boss surian....
"hivi we Cecilia una akili kweli,.. Vigezo ni kuanzia miaka 18 mwisho 35, sasa huyo mwenye miaka 58 aliambiwa hapa ni kituo cha watoto yatima kuwa aje kulea watoto??... Lete documents za vijana na nikiona documents kuanzia miaka 36 huna kazi Jinga kabisa wewe"
Simu ilikata na Cecilia akawa hana jinsi tena zaidi ya kumpa mama karatasi zake...
"mama, nimejitahidi sana kukusaidia.. Lakini nimetukanwa kama mtoto... Shika bahasha yako mama angu, ila pole sana mama..."
"boss wako ni mkali kumbe"
Aliongea mama huyo bila kujua boss huyo huyo ndio mtoto wake wa kumzaa ila anasikia sikia tu kua kafariki dunia...
Lakini sasa ikumbukwe kuwa maimuna ni jini,.. Sasa kule ndani ofisini maimuna yupo, na hapa kwa sekretari kivuli chake kipo, kwahio kule ni mwili na huku ni kivuli,... Sasa alishangaa kuona Qarina wa surian na Qarina wa huyu mama wanaongea, na yeye kama jini ndio mwenye uwezo wa kuongea na hao Qarina,.. Sasa leo maimuna ndio anajua kumbe huyo mama hapo mapokezi ndio mama yake surian, Yaani ndio mama mkwe wake kabisaa..
Je? Jini maimuna atafanya nini baada ya kujua huyo ndio mama wa mume wake ambaye ni surian??
Itaendelea...........
MWENDELEZO WA STORI HII INAPATIKANA WhatsApp Na Facebook, kwa INBOX pekee
KWA NJIA YA Facebook BONYEZA HAPA KISHA TUTUMIE MESEJI
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/
AU.... TUCHEKI KUPITIA WhatsApp, NAMBA +255714419487
Utazipata Zote Mpaka Mwisho Kwa Simu No: +255714419487 WhatsApp, Au, Like Page Yetu Ya Facebook Kwa Kubonyeza Hapa Chini ili Usipitwe
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/
tAfBoy {.Tanzania's Frugal Boy..}
0 Comment to "CHOZI LA MAMA YANGU (Masharti Ya Jini Maimuna) "
Post a Comment