Sunday, April 22, 2018

AINA KUMI ZA NDOA, KWA TANZANIA


KATIKA MAKALA YALIOPITA TULIZUNGUMZIA MASWALA YA AINA TATU ZA USINGIZI KATIKA IMANI YA KIISLAMU... leo nakujia na makala nyingine iitwayo

HIZI NDIZO AINA KUMI ZA NDOA, KWA TANZANIA



Na Dr Voice Mgosi
+255714419487 WhatsApp

1. NDOA YA MKEKA

Inatokana na kufumaniwa na Binti wa watu. Ndoa hii huwa Haina mahari. Hii huvunjika mwaka mmoja tu baada ya wanandoa kugundua hawakuwa wakipendana!

2. NDOA YA MIHEMKO

Hufungwa na vijana wenye umri wa miaka kati mume18 mke 16. Huvunjika baada ya miaka 3 au 4 ya ndoa.

4. NDOA YA MAONYESHO

Wenye ndoa Hii hupenda kujionyesha barabarani. Ila ndani hazina utii. Hupigana kila wanaporudi kutoka kwenye mizunguko. Cha kushangaza huwa hazivunjiki lakini ndiyo ndoa zinazoongoza kwa kuchepuka!

5. NDOA YA UHAMISHO

Hufungwa na watumishi wa vijijini na mjini. Ili wa kijijini ahamie mjini. Mahari hutoa anayetaka kuhamia mjini. Hata kama mahari atatoa mume lakini hii ndiyo ndoa yenye ukakasi zaidi.Huvunjika mara tu wanapoanza kuishi wote mjini. Salama ya hii ndoa ni kuhama kutoka mjini kwenda kijijini.

6. NDOA YA MIMBA

Hufungwa kwa sababu wanaoowana hawataki kuonekana makwao kuwa wamezaa nje. Au muolewaji alikuwa hampendi muoaji kwa dhati.Muoaji hutumia mimba kama mtego wa kuingia ndoani. Hii huvunjika mtoto akizaliwa na kufikisha mwaka 1.

7. NDOA YA MALI

Muolewaji miaka 18 au 28 Muoaji 65 au 70.Ndoa hii pia huitwa ndoa ya babu na mjuukuu. Ndoa ya aina hii hudumu, kwasababu mwenye kauli ni mwenye mali. Asilimia kubwa ya waume wa ndoa hizi hulea watoto wasio wao.

8. NDOA YA KWA SABABU

Hufungwa ili mradi muoaji au muolewaji aonekane tu kwa jamii kuwa naye kaoa au kaolewa. Huwa hazina utii wala upendo dhati. Ndoa ya aina hii ikifikisha miaka 4 huwa hazivunjiki wahusika huishi kwa mazoea.

9. NDOA YA UPENDO

Ndoa hizi ziliishia mwaka 1978 kabla ya vita vya Kagera. Muoaji na muolewaji hawakuangalia vitu ila utu tu ambao uliwaunganisha na kutengeneza upendo wa kudumu. Hii ilidumu miaka yote.

10. NDOA YA KUCHUMA

Ndoa hii ufungwa ili mradi muoaji au muolewaji akapate kitu au vitu fulani kutoka kwa upande mmoja wapo. Hii hudumu miaka kadhaa kutegemea na malengo ya mhusika. Wengine husubiri mpaka mhusika afe,lkn hujikuta wanakufa wao kwanza.

AHSANTE SANA NDUGU MSOMAJI KWA KUJIFUNZA NA MAKALA HII

Na Dr Voice Mgosi
+255714419487 WhatsApp

KAMA WEWE NI MPENZI WA LOVE STORY, MAMBO YA CHOMBEZO ZA HUBA, MAHABA, MKATABA, MARAHABAAAA, NA HAPA NDIO KWAO

UNAPITWAJE NA UTAMU HUU?

ORODHA YA STORI ZANGU ZOTE HII HAPA, NI BUUURE BONYEZA HAPA

www.alwayshere5.blogspot.com/search/label/CHOMBEZO

(1).KIJAKAZI WA KIUME

(2).MLINZI WA GETI

(3).DEREVA TOYO

(4).MTOTO WA HAYATI

(5).ONE DAY YES

(6).SECONDARY SCHOOL

(7).FUNDI CHEREHANI

(8).MWIGIZAJI BALAYA

(9).THE DOM

(10).THE ISLAMIC WIFE

(11).MKE JEURI

(12).YOUNG PASTOR

HIZO ZOTE, INGIA GOOGLE TAFUTA ULIO IPENDA, AU BONYEZA HAPA CHINI, UKAZISOME ZOTE, BUUURE

www.alwayshere5.blogspot.com/search/label/CHOMBEZO

AU.... Njoo WhatsApp Ujipimie....

Utazipata Zote Mpaka Mwisho Kwa Simu No: +255714419487 WhatsApp, Au, Like Page Yetu Ya Facebook Iitwayo CHOMBEZO MEDIA

tAfBoy {.Tanzania's Frugal Boy..}

Share this

0 Comment to "AINA KUMI ZA NDOA, KWA TANZANIA"

Post a Comment