Sehemu Ya 1
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/
Ilipoishia Jana →↓↓↓
MCHUNGAJI MCHANGA
NDUGU WASOMAJI WA SIMULIZI ZANGU,... KWANZA NILIANZA NA SIMULIZI YA KIISLAMU IITWAYO THE ISLAMIC WIFE (MKE MWISLAMU)... HIO INA IMANI YA DINI NDANI YAKE... HAPA KATIKATI NIKAANDIKA SIMULIZI IITWAYO NYAMA YA MAMA HIO INA IMANI YA KISHETANI... SASA LEO NALETA YOUNG PASTOR (MCHUNGAJI MCHANGA)... HII ITAKUWA NA IMANI YA DINI KAMA JINSI INAVYOJIELEZEA.... LENGO LANGU NI KUTOBAGUA SIMULIZI ZANGU ZIZIDI UPANDE FULANI... BALI ZITAKUWA PAMDE ZOTE... KAMA SIMULIZI ZANGU SIO NZURI MTANISAMEHE KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE.... NA KWENYE SIMULIZI HII KAMA KUNA VIPENGELE VIMEKOSEWA BASI TUSAMEHEANE MANA SIO UPANDE WAMGU..... AFU PIA NINGEOMBA KWAMBA KILA KINACHOANDIKWA HAPA USIKIWEKE KICHWANI... MANA HII NI HADITHI TU, HIVYO AIO KILA NENO NI KWELI... HIVYO TUSIJE TUKA PANIKI, HII NI HADITHI TU... KAMA ZILIVYO HADITHI NYINGINE.... MTANIWIA RADHI WADAU WANGU....
SASA TUANZE RASMI SIMULIZI YETU HII YA MCHUNGAJI MCHANGA
Katika kanisa moja kubwa ikiwa ni wakati wa saa nne hivi asubuhi... Kanisa kubwa lenye urefu wa rosheni mbili kwenda juu.. Na rosheni zote zimesheheni waumini wa lika mbalimbali kuanzia watoto wazee na vijana.. Wakati huo wapo mapasta ambao walikuwa wakitoa sifa kwa Bwana Yesu kwa kutumia nyimbo za injili,... Floo ya chini ya kanisa hilo ni sehemu ya kupaki magari, na floo ya katikati ni ukumbi mkubwa yaani kama kuna ndoa basi hapo ndipo mahali pake, ila pia hio floo ya katika imejaa waumini, mana sio siku zote watu wanaoa, na pia ina skrini kubwa karibia ukuta mzima ule wa mbele, hio ni skrini ya kumuonyesha pasta akiwa floo ya juu, yaani ni kama sinema vile,,.. Sasa hio floo ya juu na ya mwisho, ndio kanisa lenyewe,.. Ukiangalia mazabauni yaani imeng'aa kwa maru maru maalum, yaani pale ni sehemu ya pasta pekee. Na wakati huo pasta bado hajaja, hivyo waumi waikuwa wakitoa sifa za bwana Yesu kwa kupitia nyimbo zilizoimbwa na wasanii mahiri nchini,
Sasa huku chini ilionekana gari moja ya bei mbaya... Ikiwa inapaki, tena ina sehemu yake maalum ya kupaki sio kila mahali,... Ilikuwa ni familia moja iliokuwa ikija kanisani, na ilionekana kuheshimika sana kanisani hapo,... Walikuwa ni wasichana watatu waliotofautiana umri, akiwemo baba yao na mama yao,... Hatua za kuelekea kanisani zilianza taratibu, na kila muumini aliiheshim familia hio,...
"tumsifu yesu Kristo"
Ni waumini waliokuwa wakitoa salamu kwa bwana huyo, huku akiwaitikia
"milele amina"
Yaani waumini wanapanda kwa ngazi, lakini yeye ana lift yake maalum, yaani yeye na familia yake hutumia wao tu,... Alipofika ndani ya kanisa waumini wote wa floo ya katikati na floo ya mwisho walinyanyuka na kutoa salamu kwa pamoja...
"tumsifu Yesu Kristo alie hai mbele za mungu"
Walisema waumini hao huku familia ikiwa ina viti vyao pale mbele, yaani ule ule upande wa waumini, sasa viti vya mbele ni spesho kwa ajili ya familia hio... Lakini pia katika viti hivyo kuna kiti kimoja hakikuwa na mtu, na ni kiti cha mmoja wa familia hio na hakiruhusiwi kukaliwa.... Sasa hatujui huyo aliosalia kukaa pale ni nani,.... Pale pale mr huyo alipanda mazabauni,....
Kumbe huyo bwana ana kipawa cha UBISHOP yaani ni Bishop Jacob... Ni kiongozi wa makanisa yake yapatayo 50 kwa idadi kamili.... Yaani mzee huyu ana makanisa 50 makubwa kama hili na ni yakwake peke yake... Anayasimamia mwenyewe, licha ya kuwa Bishop, bado pia ni tajiri mkubwa... Mana ana makampuni mengi sana, ana viwanda... Huezi amini ni Bishop anaemiliki ndege binafsi, ana magari ya kutembelea kama utitiri,.....
"tumsifu Yesu Kristo kwa jina la baba"
Aliongea Bishop Jacob huku waumini wakipaza sauti zao kwa hali na mali
"milele aminaaaaaa"
Raha sana ukiwa na imani ya dini yako....
Wadada, wamama, wakaka, watoto, wazee.... Yaani malika yote yalijaa hapo, na unambiwa akitoka hapo anakwenda katika makanisa mengine kutoa neno la bwana... Yaani amekuwa mtu wa kutoa neno siku nzima....
BISHOP ni kipawa au cheo kikubwa ambacho ni ukitoka pasta sasa anaefatia kwenda juu,... Anakuwa ni Bishop, lakini pia Bishop ana mkubwa wake ambaye ni ATBISHOP huyu ATBISHOP huyu sio mtu wa kawaida, huyu anaweza kuwa ATBISHOP wa kidunia au wa kitanzania nzima.... Yaani anasimamia au kuongoza makanisa yote Tanzania. Na sio kuwa ni yake lahasha bali anayasimamia tu, na pia sio kuwa anasimamia yote, lahasha bali kuna matawi mengi sana juu ya haya makanisa... Hivyo atasimamia makanisa ambayo ni tawi fulani pekee, hivyo atakuwepo ATBISHOP mwingine wa kusimamia makanisa ya tawi lake husika... Hivyo ATBISHOP ni mkubwa, tuchukulie mfano wa rais.... Afu huyu Bishop yeye tufanye ni kama mbunge... Hivyo katika mkoa mmoja kunaweza kuwa na ma Bishop hata mia moja.. Kutokana na kila mtu kumiliki jimbo lake yaani makanisa yake.... Nakupa tu kwa ufupi ujue vipawa vilivyo....
Sasa Bishop Jacob alianza kuhubiri kama ilivyo kawaida yake, ni mchungaji aliojaaliwa kipawa na upako wa hali ya juu katika kutoa neno la Bwana,.... Waumini walikuwa wakilia kutokana uzito mahubiri aliokuwa akihubiri Jacob,... Machozi kila muuni, wengine kama kawaida yao kudondoka chini wakati wa pepo kutoka,... Na yote hayo ni kwasababu ya mchungaji Jacob au Bishop Jacob
ILANI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO
TAFADHALI SANA KWA WEWE UNAEKOPI SIMULIZI HII BILA IDHINI YA MMILIKI,... HURUHUSIWI KUIFANYIA CHOCHOTE KAMA VILE, KUUZA, KUKOPI, NA VINGINE... HATUA KALI ZITACHUKULIWA, KWA KIFUNGU CHA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA MITANDAO,... HAKIKISHA UNA KIBALI MAALUMU CHA KUFANYA HIVYO, LAA SIVYO NI KOSA LA KIMTANDAO KWA KUHUJUMU KAZI ISO YAKWAKO....
NDUGU MSOMAJI, HAKIKISHA ANAEKUUZIA SIMULIZI HII NI MMILIKI HALALI MWENYE NAMBA HII, +255714419487.. Sharbiny Rashidy Kingazi... LAA SIVYO NAWE NI MMOJA KATI YA WAHUJUMU WA KAZI ZA WATU, KATIKA MITANDAO...
WALE WA KUPESTI MITANDAONI HAKIKISHA, UNAPATA IDHINI KUTOKA KWA MMILIKI HUSIKA KWA SIMU NO, +255714419487 WhatsApp
ILI UPATE MAELEZO, VIGEZO, NA MASHARTI YA KUFANYA HIVYO,.. TAFADHALI SANA HATUPO KWA AJILI YA KUINGIZANA PABAYA KISHERIA... TUWE MAKINI NA HILI...
Mahubiri yaliisha na hatimaye ibada ya siku ya Jumapili inakwenda ukingoni,... Lift yake ni ile ile, hachanganyikani na waumini hata siku moja,.... Akiwa na familia yake wanaingia katika gari,.... Lakini wakati wanaingia alitokea mschana mmoja ambae nae ni muumini wa kanisa hilo,..
"tumsifu yesu Kristo mama"
Alisalimia mschana huyo huku akimpa mkono mke wa Jacob,....
"milele amina..... Eva mbona siku hizi huji nyumbani, au kwasababu mwenzio hayupo"
Aliongea mama huyo aliokwenda kwa jina la Rebecca,.. Sasa hatukujua huyo mwenzie ni nani haswa, lakini eva alipokua akisalimiana na mwanamke huyo, ghawna wale wasichana nao wakaanza kumsalimia eva....
"heee wifi hali yako"
Aliongea mtoto mkubwa wa huyo mama aliokwenda kwa jina la Jessica mwenye umri wa miaka 28, ndio mtoto wa kwanza kwenye hio familia, lakini sasa Jessica kamuita eva wifi kitu ambacho hatujui kaolewa na ndugu yake nani, au ndio ile utani tu,... Mara mschana mwingine kasalimia
"shkamo wifi eva"
Alisalimia mschana mwingine aliokwenda kwa jina la martha, mwenye umri wa miaka 20.... Kuna mwingine hakutaka kuachwa nyuma kwa salamu
"wifi eva shkamo"
Alisalimia mschana mwingine wa mwisho, aliokwenda kwa jina la maria ana miaka 15...
"amarahaba mawifi zangu hamjambo"
"hatujambo... Hatukuoni nyumbani"
"aahhh nitakuja Maria usijali"
Eva alikuwa ni mschana mzuri sana na mwenye heshima kwa rika zote,
"mwanangu, kabla mwenzio hajakwenda masomoni, ulikuwa unakuja, lakini sasa hivi huuuji jamani"
Aliongea Rebecca au mama Jessica, au mama mchungaji,...
"mama, hata mimi hua nakuwa na ubize sana... Sasa hivi nadili sana maombi, sitaki mwenzangu anikute nipo nyuma, hivyo nami nakua bize na mungu"
"yesu atakubariki eva,... Na naomba nikutaarifu, mwenzio anarudi wiki ijayo"
Eva kusikia mwenzie anarudi wiki ijayo, alifurahi na kuruka ruka, alimkumbtia mama mkwe wake karibu kudondoshana, mpaka baadhi ya waumini walishangaa kwa furaha hio alionayo eva...
"eva utaniangusha jamani"
"mama, nina furaha kiasi gani juu ya taarifa hio"
Eva ana mdogo wake wa kike aitwaye HAPPINESS, mwenye miaka 15 alikuja pale baada ya kuona dada yake ana furaha...
"tumsifu yesu Kristo mama"
Alisalimia happy huku akiinama chini kuashiria ni heshima ya hali ya juu mno,...
"milele amina,... Heew happy, umependeza Jumapili ya leo"
"ahsante mama... Sifa kwa Yesu"
"amina mwanangu"
Basi waliongea mengi sana na hatimae kila mmoja kuondoka baada ya ibada kuisha,...
Kuanzia hapo Eva alikuwa ni mtu wa furaha siku zote, mana sasa usingizi wake karibu kuja... Eva ni mschana aliolelewa katika mazingira ya kidini na anaijua dini haswa, yaani humwambii kitu kuhusu Bibilia,... Eva alipofika nyumbani alimkuta mama yake kesharudi, nyumbani... Ni familia ya kawaida sana...
"mamaaaa..... Yesu kajibu maombi yangu mama"
Aliongea eva huku akimkumbatia mama yake,...
"ni nini eva... Afu leo sijakuona kanisani ulikaa wapi"
"mama... Leo niliamua kukaa nyuma sana"
"enheee, yesu kajibu maombi yako kivipi... Mana una furaha kweli yani"
Aliongea mama huyo huku mama akiwa anaandaa ratiba zake za jumuiya,..
"mama njoo ndani nikwambie"
Mama eva aliingia ndani ili kumsikiliza mtoto wake...
"haya Niambie"
"mama.... Wiki hii mkwe wako anakuja"
Mama alishangaa kusikia mkwe wako anakuja....
"ina maana umeachana na adam unataka uniletee mwanaume mwingine, eva mwanangu ni mawazo gani unayo"
Mama alikuwa hajamuelewa mtoto wake ana maana gani...
"mama sio kuwa naleta mwanaume mwingine,.... Namaanisha huyo huyo Adam, anarudi toka masomoni"
"weeeee.... Unasema kweli"
"ndio,.. Nilikuwa na mama mkwe pale kanisani ndio kaniambia"
"jamani eva mwanangu"
"nini mama.... "
Familia hio ni familia fukara sana ila wengi wao wanaona wivu kwa mtoto Bishop Jacob, kuoa katika familia hio, na ni kila muumini anajua uhusiano wa Adam na Eva,... Lakini kwakuwa Eva anaishi katika maisha ya kimasikini hivyo kwao ni kama bahati kuolewa na mtoto wa kitajiri, tena mtoto wa Bishop, yaani sio pasta ni Bishop... Kwa wale waikristo nikisema Bishop nadhani mnanielewa..
"mara paaap adam anashuka kwenye ndege na mke wa kinaigeria... Utafanyeje sasa"
Mama alimwambia mwanae hivyo mana adam yupo Lagos nchini Nigeria, katika vyuo vya dini ya kikristo, japo adam ana nguvu na miujiza kuliko hata baba yake, lakini akaamua kwenda kujiongeza, sasa akirudi huko ni moto wa kuotea mbali, Sasa baada ya mama eva kusema hivyo, eva alianza kulia huku akisema kuwa....
"mamaaaaaa..... Usiseme hivyo"
"sikuombei umkose mwanangu... Ila wanaume wa siku hizi.... Siwawekei mia kwa mia... Hawakawiii kubadirika"
"ni kweli mama... Lakini sio kwa mtu mwenye imani kama adam"
"eva mwanangu, mimi ni mama yako... Nimekuficha mengi sana kuhusu adam.... Na nikisema nikuambie nitakupoteza mwanangu... We mpende tu"
Eva alitoa jicho kuskia mama yake anasema maneno hayo.....
"unasemaje mama"
"una kifua cha kubebea jambo mwanangu, tusije kuanza kupepeana na kanga hapa"
Aliongea mama yake eva huku wakikaa vizuri kitandani
"mama... Nipo tayari kumwacha adam kama ana tabia chafu"
"heeeeee wewe ndio wa kusema hivyo"
"mamaaaaa Niambie basi nijue"
BONYEZA HAPA CHINI..... ↓↓↓
www.facebook.com/Chombezo-Media-571095712946246/
BILA SHARE 300 NA LIKES 500
MTASUBIRI NDANI YA SIKU TANO
AU.... Njoo WhatsApp Ujipimie....↓↓↓
Utazipata Zote Mpaka Mwisho Kwa Simu No: +255714419487 WhatsApp, Au, Like Page Yetu Ya Facebook Kwa Kubonyeza Hapo Juu..→↑↑↑
tAfBoy {.Tanzania's Frugal Boy..}
0 Comment to "YOUNG PASTOR Sehemu Ya 1"
Post a Comment