Thursday, January 11, 2018

WANAUME TUSIYAFANYE HAYA KWA WAKE ZETU, HAIFAI

WANAUME TUSIYAFANYE HAYA KWA WAKE ZETU, HAIFAI

Mwandishi: Dr Voice Mgosi

Simu No, +255714419487 WhatsApp

TUYAZINGATIE MAKATAZO HAYA KWA NDOA BORA NDANI YA NYUMBA ZETU.



1, Usitangaze udhaifu wa mkeo kwa familia na marafiki, kila mmoja
anamtunzia mwenziwe hadhi yake.

2, Usiwe na mtizamo mbaya wala kuzungumza naye kwa hisia kali
huwezi kujua atatafsiri vipi.!

3, Usimlinganishe mkeo na wanawake wengine, huwezi kujua hao wanawake
wengine wanapitia hali gani kimaisha. Kila mwanamke anasifa zake.

4, Usisahau kwamba ni mkeo umemuoa, yeye si kijakazi, muhudumie kama malikia na atauonyesha ulimwengu kwamba
Mumewe ni mfalme na utamtawala maishani.

5, Mpe kipaumbele na ni wajibu wako binafsi kumfanyia jambo na sio watuwengine.

6, Usimlaumu mbele za watu hata kama kakosea, mlinde, muhimize, mrekebishe faraghani, ukifanya hivyo kamwe hatokusahau.

7, Usimnyime huduma za kitandani kwa kujifanya mgonjwa/kuchoka ama
kutokuwa na hamu. Kumbuka wanaume wengine wanatafuta nafasi
hiyo.

8, Usimlinganishe mkeo na mtalaka wako ama mkeo aliyefariki maana wewe ni mume wa pekee kwake.

9, Usimkemee wala kumkosoa mbele
ya watoto, ni malezi mabaya kwa watoto maana wewe ni Mwalimu wao, wanakutazama wewe japo unadhani ni watoto tu!.

10, Mtazame mkeo kama kavaa vizuri kabla hajatoka maana akipendeza yeye na wewe unaheshimika na
ukipendeza wewe yeye anaheshimika.

11, Usikubali marafiki kuwa karibu na mkeo, weka mipaka maana hujui nia
zao.

12, Usitoke kuoga na haraka haraka ukavaa nguo ukatoka pasi yeye kukukagua, mkeo kazungukwa na wanaume wanadhifu wanaojali
mazavi na utanashati.

13, Wazazi, ukoo na marafiki sio waamuzi kwa mambo ya mkeo,  usipoteze muda kutafuta uamuzi wa
mwisho kutoka kwao, ithibiti Ndoa yako.

14, Mapenzi yako yasiwe kwa sababu ya mazingira au kihali hata kama ulimuoa kwa misingi hiyo kwa sasa ni
mkeo mpende bila masharti. Hali uweza kubadilika na ikiwa ndio msingi
basi ndoa itavunjika.


15, Mkeo anahitaji umakinike kwake na umsikilize kama mtoto, usiwe mkali msikilize kwa makini na atakupenda.

16, Usijilinganishe na mkeo, yeye ni mke kwa hivyo msaidie tu maanandoa ni kusaidia.

17, Usimuhukumu mkeo, ni msaidizi wako na kiumbe dhaifu mchukulie kwa mtazamo huo na utapata utulivu wa akili.

18, Mume mzembe hajali. Haogi. Jiweke nadhifu ukiwa na yeye nukia vizuri, harufu mbaya inamkirihisha ila
hawezi kukwambia.

19, Usiwe na urafiki na waume walio na mtazamo mbaya kuhusu Ndoa, Watakuharibu mawazo.

20, Mkeo ana thamani kubwa sana ndio maaana ukatoa vitu vya thamani
kumuoa. Penzi lenu lifanye jipya, uzembe haufai.

21, Kuzaa ni majaaliwa, mpende mkeo awe na watoto au asiwe nao,
usiwabague watoto kwa jinsia wafunze dini na watakuwa wacha
Mungu hadi maishani mwao.

22, Hauwi mzee kwa mkeo katika kumburudisha, usiwe na ugomvi naye
mutakuwa katika kheri. Usiwache kuwajali watoto wako na mkeo kwa
sababu ya wanawake wengine au sababu yoyote ile. Wao ni wewe na
wewe ni wao.

23. Mume anayedumu na ibada ana usalama, omba kila siku, muombee
mkeo na watoto.

TUYAZINGATIENI HAYA TUWE NA NDOA BORA KATIKA NYUMBA ZETU

Na Dr Voice Mgosi +255714419487

UNAPITWAJE NA UTAMU HUU?

ORODHA YA STORI ZANGU ZOTE HII HAPA, NI BUUURE KUPITIA HAPA

www.alwayshere5.blogspot.com/search/label/CHOMBEZO

(1).KIJAKAZI WA KIUME

(2).MLINZI WA GETI

(3).DEREVA TOYO

(4).MTOTO WA HAYATI

(5).ONE DAY YES

(6).SECONDARY SCHOOL

(7).FUNDI CHEREHANI

(8).MWIGIZAJI BALAYA

(9).THE DOM

(10).THE ISLAMIC WIFE

(11).MKE JEURI

(12).YOUNG PASTOR

HIZO ZOTE, INGIA GOOGLE TAFUTA ULIO IPENDA, AU BONYEZA HAPA CHINI, UKAZISOME ZOTE, BUUURE

www.alwayshere5.blogspot.com/search/label/CHOMBEZO

AU.... Njoo WhatsApp Ujipimie....

Utazipata Zote Mpaka Mwisho Kwa Simu No: +255714419487 WhatsApp, Au, Like Page Yetu Ya Facebook Iitwayo CHOMBEZO MEDIA

tAfBoy {.Tanzania's Frugal Boy..}

Share this

0 Comment to "WANAUME TUSIYAFANYE HAYA KWA WAKE ZETU, HAIFAI "

Post a Comment